Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori amenzindua mradi wa maji wa Mtaa wa Msakuzi Kata ya Kwembe  utakaohudumia kaya 3500 za eneo hilo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mradi huo, Makori amesema kuwa anawapongeza Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) kwa hatua kubwa waliyoifanya ya kuleta maji katika eneo la Mtaa huo.

Makori amesema, kupatikana kwa maji kwenye eneo hili litaondoa kero ya maji iliyokuwa inawasumbua wananchi kwa muda mrefu. Mkuu wa Wilaya ameweza pia kuzindua vizimba vitatu vitakavyohudumia wananchi 18,000 kwa kwa siku na pia itasaidia kwa wale ambao hawatakuwa wameunganishwa.

Akiongea kwa niaba ya DAWASA Meneja wa Mkoa wa Ubungo Mhandisi Pascal Fumbuka amesema Mradi wa Mtaa wa  Msakuzi wa Km 2.1 utahudumia kaya kaya 3500 sawa na wananchi zaidi ya Laki mbili (200,000) wa eneo lote na mpaka sasa wananchi 500 wameshajaza fomu bado kuunganishiwa maji tu.

Kuongezeka kwa wateja wa eneo la Mtaa wa Msakuzi, Fumbuka amesema wanatarajia kuongeza pato la Kimkoa na kufikia Bilion 1.5 kwa mwezi na pia wizi wa maji utapungua baada ya wananchi wa eneo hilo kuunganishiwa maji. Ameeleza kuwa huduma ya kuunganishiwa maji wananchi ni la mkopo na utaandikishwa mkataba baina ya DAWASA na mwananchi ambao utalipwa ndani ya mwaka mmoja.
 

DAWASA wanaendelea kuboresha huduma za upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waliokuwa nje ya mradi kwa muda mrefu na kuwapelekea huduma hiyo muhimu ambapo wananchi wengi wameshukuru jitihada zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Mkuu wa Wilaya Kisare Makori akimtua ndoo ya maji mama kichwani baada ya kuzindua kizimba cha maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Mtaa wa Msakuzi Kata ya Kwembe utakaohudumia na kuwanufaisha wananchi zaidi ya laki mbili (200,000).
Mkuu wa Wilaya Kisare Makori akizungumza na wananchi waliojitokeza wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wa Mtaa wa Msakuzi Kata ya Kwembe  utakaohudumia na kuwanufaisha wananchi zaidi ya laki mbili (200,000).
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kisare Makori akizindua moja ya kati ya vizimba vitatu vilivyopo katika mradi wa maji wa Mtaa wa Msakuzi Kata ya Kwembe utakaohudumia na kuwanufaisha zaidi ya wananchi laki mbili kwa siku (200,000).
Meneja wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (DAWASA) Mhandisi Pascal Fumbuka akielelezea mradi wa maji wa Mtaa wa  Msakuzi Kata ya Kwembe na wakiendelea kuwaunganishia maji wananchi waliokwisha jaza fomu ili kupata huduma ya majisafi na salama.

Wananchi wa eneo la Mtaa wa  Msakuzi Kata ya Kwembe  wakiendelea kujipatia huduma ya maji katika moja ya Kizimba kilichopo eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...