Mkuu wa Wilaya huyo Ndugu Jerry Muro akizsisikiliza changamoto za 
Wananchi zaidi ya 260 katika kata ya bwawani Halmashauri ya Arusha , wilayani Arumeru Mkoani Arusha waliokuwa kwenye hatari ya kusombwa na mafuriko kufuatia nyumba zao kuanza kutitia chini ya Ardhi .Mkuu wa Wilaya huyo Ndugu Jerry Muro akizsisikiliza changamoto za 
Wananchi zaidi ya 260 katika kata ya bwawani Halmashauri ya Arusha , wilayani Arumeru Mkoani Arusha waliokuwa kwenye hatari ya kusombwa na mafuriko kufuatia nyumba zao kuanza kutitia chini ya Ardhi .

Wananchi zaidi ya 260 katika kata ya bwawani Halmashauri ya Arusha , wilayani Arumeru Mkoani Arusha waliokuwa kwenye hatari ya kusombwa na mafuriko ambapo zaidi ya nyumba 100 zilianza kutitia chini ya ardhi wamesaidiwa na Mkuu wa Wilaya huyo Ndugu Jerry Muro kutolewa katika makazi yao ya awali ambayo yalikuwa hatarishi na kupelekwa katika maeneo mengine mazuri na Salama .

Wakizungumza katika ziara maalumu ya Mkuu wa wilaya Hiyo Ndugu Jerry Muro,wananchi hao wameeleza adha wanayokumbana nayo katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuishi kwenye nyumba ambazo kwasasa ni kama vibanda kutokana na kutitia kwa sababu ya mafuriko, wamesema kuwa wapo katika hatari kubwa na kuiomba serikali kuwatafutia namna ya kuwahamisha katika maeneo hayo

Kufuatia kilio cha wananchi hao ambao wanaishi katika shamba la mwekezaji Lusy Estate ambaye anaishi katika eneo hilo kwa ajili ya kilimo cha mkonge,Mwenyekiti wa ulinzi na usalama katika wilaya hiyo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro akatoa agizo la kuhama kwa wananchi hao ndani ya juma moja ili kuzinusuru familia zao.

"Familia hizi ambazo zinaishi katika eneo hili,ni waajiriwa katika shamba la Lus estate kwa ajili ya Kilimo cha Mkonge,ambapo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya mafuriko huku wengine wakilazimika kuyakimbia makazi yao ,ambapo sasa huenda wakanusurika kutokana na agizo hilo la mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama.",alisema DC Muro.

 Mkuu wa Wilaya huyo Ndugu Jerry Muro akizsisikiliza changamoto za
Wananchi zaidi ya 260 katika kata ya bwawani Halmashauri ya Arusha , wilayani Arumeru Mkoani Arusha waliokuwa kwenye hatari ya kusombwa na mafuriko kufuatia nyumba zao kuanza kutitia chini ya Ardhi .
  Mkuu wa Wilaya huyo Ndugu Jerry Muro akikagua baadhi nyumba  za
Wananchi zaidi ya 260 katika kata ya bwawani Halmashauri ya Arusha , wilayani Arumeru Mkoani Arusha zilizopo kwenye hatari ya kusombwa na mafuriko kufuatia nyumba zao kuanza kutitia chini ya Ardhi .
 Mkuu wa Wilaya huyo Ndugu Jerry Muro akizungumza na baadhi ya Wananchi zaidi ya 260 katika kata ya bwawani Halmashauri ya Arusha , wilayani Arumeru Mkoani Arusha waliokuwa kwenye hatari ya kusombwa na mafuriko kufuatia nyumba zao kuanza kutitia chini ya Ardhi . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...