Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Mkoa Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika mjini Njombe.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Bumi Mwamasage akieleza lengo la Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto kukutana wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika mjini Njombe.
Kiongozi wa Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Hanifa Selengu akieleza lengo la timu hiyo kwenda mkoani Njombe wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika mjini Njombe.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Denis Bashaka akileza namna Sheri ya uchawi sura ya 18 ya Mwaka 2002 inavyozuia vitendo vya upigaji ramli na kazi za uganga wa kienyeji wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto kilichokutana Mjini Njombe

Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Mwanaisha Moyo akielezea umuhimu wa Kamati hiyo kutoa huduma kwa wahanga wa vitendo vya ukatili kwa haraka wakati wa kikao cha Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto kilichokutana Mjini Njombe.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Mkoa wa Njombe ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto wakiongozwwa na Mkuu waWilaya ya Njombe kwa niaba ya Mkuu wa mkoa Ruth Msafiri (wa pili kulia) wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa kikao cha Kamati hiyo kilichofanyika mjini Njombe.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

………………………..

Na Mwandishi Wetu Njombe

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amemuagiza Katibu Tawala wa Wilaya hiyo na watendaji wote kuzunguka katika mitaa kubandua mabango yote yanayotangaza huduma za waganga wa kienyeji ambao wanafanya kazi kinyume cha Sheria.

Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na Kamati ya Mkoa wa Njombe Ulinzi wa Mwanamke na Mtoto kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa na kusisitiza kuwa hatovumilia vitendo vya ukiukwaji Sheria ya Uchawi Sura ya 18 ya mwaka 2002 inayokataka upigaji ramli na kujihusisha na masuala ya kishirikina.

Ameongeza kuwa Serikali haitovumilia vitendo vyovyote vinavyojihusisha na masuala ya kishirikina kufanyika katika Wilaya ya Njombe kwani vimekuwa vikisababisha mifarakano na taharuki kubwa na kupelekea kutokea kwa utekaji na mauaji katika jamii.

Mkuu wa Wilaya huyo amesema kuwa baadhi ya watendaji wa Serikali za Mitaa na vijiji wamekuwa wakishiriana na waganga wa kienyeji kutekeleza masuala yanayohusishwa na imani za kishirikina.

“Nimemuagiza Katibu Tawala wa Wilaya kushusha agizo hili kwa watendaji wa vijiji na mitaa na sitaki kuyaona mabango hayo na nikiyaona tena nitachukua hatua kali za kisheria kwa watakaobainika kuyaweka” alisema

“Niseme tu sitosita kuwachukulia hatua watendaji watakaoendelea kushirikiana na waganga wa kienyeji na kuwakaribisha katika vijiji na mitaa yao na kuwasaidia kufanikisha kazi zao ambazo ziko kinyume cha Sheria” alisema

Mkuu huyo wa Wilaya ameomba ushirikiano kutoka kwa Kamati za Ulinzi wa Mwanamke na Mtoto kuanzia ngazi ya mkoa na Halmashauri ili kusaidiana katika mapambano ya kutokomeza vitendo vya ukatili kwa watoto.

Akizungumza katika kikao hicho kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Bumi Mwamasage amesema kuwa Kamati hiyo inatakiwa kuwajibika katika jamii kwa kutoa elimu na ishuke kwa jamii ili kuwawezesha wanajamii hao kuunga mkono mapambano ya vitendo vya kikatili dhidi ya Mwanamke na Mtoto.

Kwa upande wake Kiongozi wa Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Hanifa Selengu amesema kuwa Wizara imeamua kushirikiana na Mkoa wa Njombe kwa kuitisha Kamati ya Ulinzi wa Mwananmke na Mtoto ili kujadili kwa pamoja na kupata namna bora ya kupambana na kutokomeza vitendo vya kikatili kwa mwamake na Mtoto.

“Tumekuja kuongeza nguvu katika masuala haya yaliyojitokeza Mkoani hapa kwani wote tunadhamana ya kumlinda Mtoto dhidi ya vitendo vya kikatili” alisema. Naye Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Mwanaisha Moyo amesema kuna umuhimu wa Kamati hiyo kutoa huduma kwa wahanga wa vitendo vya ukatili kwa haraka na kwa wakati.

Aidha Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Denis Bashaka namna Sheria ya Uchawi Sura ya 18 ya Mwaka 2002 inavyozuia vitendo vya upigaji ramli na kazi za uganga wa kienyeji ambavyo vinahusishwa na mauaji yaliyojitokeza mkoani Njombe.

Kamati ya Ulinzi kwa Mwanamke na Mtoto ya Mkoa wa Njombe imekutana Mjini Njombe kujadiliana na kupata namna bora ya kuondokana na vitendo vya kikatili hasa vitendo vya utekaji na mauaji ya watoto mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...