Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.

MKURUGENZI wa Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema juhudi mbalimbali za wadau wakiwemo mashahidi pamoja na mawakili wa pande zote mbili  katika kesi ya kujihusisha na mtandao wa uhalifu wa nyara za serikali, Yang Glan maarufu Malkia wa Meno ya tembo  wenzake ndizo zimefanikisha washitakiwa hao kutiwa hatiani . 

Ameyasema hayo leo Februari 19, 2019 wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ambapo amesema ni muhimu kwa wadau wote nchini  kuongeza ushirikiano katika mapambano dhidi ya vitendo vya ujangili ambavyo kwa kiasi kikubwa vimelisababishia taifa hasara hasa katika upotevu wa maliasili muhimu hususani wanyamapori kama tembo na wengineo. 

 Amesema Watanzania wanapaswa kuzilinda maliasili zote zilizopo nchini kwani wakishindwa kufanya hivyo ipo hatari ya kupotea na watalii kutokuja tena Tanzania hali itakayosababisha pato la taifa kushuka.

Hata hivyo, amesema kwa upande wa kiuchumi madhara yatokanayo na ujangili na biashara haramu ya nyara za serikali hususani meno ya tembo ni mengi hiyo ni kutokana na ukweli kuwa takribani asilimia 17.5 ya pato la taifa inatokana na shughuli za kiutalii. 

Ameongeza kuwa, ni ukweli usiopingika kuwa watalii wengi huja Tanzania kwa lengo la kuangalia wanyamapori ambapo mnyama anayeongoza kwa kuvutia watalii hao ni tembo. Takwimu zinaonesha kuwa sekta ya utalii ndiyo inayoongoza kwa kuingiza fedha za kigeni nchini na asilimia 90 ya mapato ya utalii nchini utegemea utalii wa wanyamapori. 

Awali, akielezea thamani ya meno ya tembo, Ofisa wa Wanyamapori kutoka Idara ya Wanyamapori iliyopo Wizara ya Maliasili na Utalii, Kiza Baraga (37) alisema amekuwa akifanya tathmini ya wanyamapori waliouawa na majangilu au wanaofanya biashara haramu ya meno ya tembo.

Alisema wapo tembo wa aina mbili ambao wanapatikana kwenye misitu na maeneo ya wazi na kwamba meno ya tembo 860 ni sawa na tembo wazima 430 ambapo  mmoja ana thamani ya dola za Marekani 15,000.

"Tembo anasaidia Wanyamapori wengine kuishi kwa kuangusha misitu, kuondoa vichaka na miiba ambapo swala na nyumbu wanajipatia chakula kwa urahisi," alisema Baraga.

Pia alisema ujangili unaathari kubwa kwa sababu wanapouawa huchangia wanyama wengine huondoka  hivyo kuwindwa na kuuwawa.

Aidha amesisitiza ujangili wa tembo husababisha kuingizwa silaha haramu za kivita ambazo hutumika kuwindia wanyama hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...