Anaandika Abdullatif Yunus – Missenyi, Kagera.

Shirika la chakula Duniani FAO linalotekeleza mradi wa kurejesha hali kwa Wakulima waliopatwa na majanga mbalimbali kwa kushirirkiana na Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi Mkoani Kagera, Lipo katika hatua za mwisho kukamilisha mradi huo ulioanza tangu Mwaka 2017, unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu huku mradi huo ukionekana kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mapema Akizungumza na waandishi wa habari Februari 11, 2019 wakati wa Kampeni ya Lishe na Mafunzo ya usindikaji, Kaimu Mratibu wa Mradi huo Bwn. Amoni Lugeiyamu ambae pia ni Afisa Kilimo Wilayani Missenyi, mafunzo yaliyofanyika katika kijiji cha Nyankere, amethibitisha juu ya Mafanikio hayo ambapo amesema kuwa, FAO Kupitia Halmashauri ya Wilaya Missenyi chini ya Timu ya wataalamu kutoka katika Idara ya Kilimo na Maendeleo ya jamii pamoja na kitengo kinachoshughulikia masuala ya lishe na Udumavu, mpaka sasa wamefanikiwa kuwajengea uwezo Wakulima kupitia semina na mafunzo mbalimbali, kugawa Vipando, Mbegu, Kuku na Vifaranga vya Samaki, Kutoa Elimu ya Lishe kwa Vijiji vinne, Kutekeleza Kampeini ya Lishe na Usindikaji kwa Vijiji Vinne vinavyolengwa na mradi huo, kuongeza uhakika wa chakula kwa kaya lengwa, sambamba na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kinga njaa (mihogo na viazi).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanufaika wa mradi huo wameshukuruku Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya Missenyi kuwa nao bega kwa bega kwa kipindi chote tangu kutokea kwa majanga hayo, na zaidi kuonekana kufurahishwa na uzalishaji wanaofanya kwa sasa lakini kubwa ikiwa ni elimu na mafunzo mbalimbali ambayo wamekuwa wakipatiwa, ambayo yamekuwa chachu ya kufikia malengo ya mradi. 

 Kwa Wilaya ya Misenyi tayari FAO wametekeleza kwa Mafanikio makubwa Mradi Huo kwa Kuzifikia kaya za Wakulima zipatazo 709 Ndani ya Vijiji (5) vya Minziro, Karagala, Kikono, Nkerenge na Nyankere, ambapo wanufaika wa mradi huo ni pamoja na Vikundi vya Kijamii, akina mama, wajasiliamali, wafugaji, na Wakulima kwa jumla yake ni Vikundi 20.

Mradi kama huo pia unatekelezwa katika Wilaya za Bukoba Manispaa, Bukoba Vijijini, Kyerwa na Muleba hivyo kufanya jumla ya Wilaya (5) ndani ya Mkoa wa Kagera. Wilaya hizo ni zile ambazo kwa kiasi kikubwa zimekumbwa na majanga mbalimbali Mkoani Kagera , yakiwemo yale ya Ukame, Mvua, Tetemeko, na Magonjwa ya mimea.
Bi. Nailath Idrisa (63) Mkazi wa Kijiji cha Nyankere akifanya majaribio ya kukata kukata Viazi lishe kwa kutumia mashine maalumu wakati wa mafunzo yanayotekelezwa na FAO kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Missenyi.
Pichani ni Mwezeshaji wa Mafunzo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Bi Zenath Hassan (Mratibu wa lishe) akiendelea kufundisha masuala ya lishe kwa Wakazi na Kijiji cha Nyankere Wilayani Misenyi.
Pichani Ni Kaimu Mratibu wa Mradi wa FAO Bwn. Amon Lugeiyamu (Afisa Kilimo, Missenyi) akizungumza na Vyombo vya Habari juu ya Mafanikio ya Utekelezwaji wa mradi wa urejeshaji hali kwa Wakulima na Wafugaji waliopatwa na Majanga Wilayani Missenyi Mkoani Kagera.
Pichani anaonekana BIi. Godbeltha Reveliani (53) Mkazi wa Kitongoji Kigarama Kata Mabale, akifurahia somo la usindikaji na utengenezaji chichili, katika Kampeni ya Lishe na Usindikaji, pembeni ni rafiki yake Bi. Grace John (54).
Pichani ni Bwn. Abdulkadiri Biligenda (44) Mkazi wa Nyankere akisaidiwa na mkufunzi wa mafunzo hayo Bw. Fredrick Kitone jinsi ya ukataji wa viazi lishe katika vipande vidogo (crips) tayari kwa kukaangwa na kuliwa.
Pichani baadhi ya akina mama kutoka Vikundi mbalimbali kaya tofauti Kijiji Nyankere, Wilayani Missenyi, wakimenya Viazi lishe tayari kwa usindikaji, wakati wa mafunzi ya lishe yaliyortibiwa na FAO kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Missenyi Februari 11, 2019. (Picha zote na Abdullatif Yunus).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...