Baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 bora katika ligi ya Europa alhamisi iliyopita, Arsenal watakuwa jijini London katika uwanja wao wa nyumbani, Emirates Stadium kukabiliana na BATE Borisov katika mechi ya marudiano ya kufuzu hatua ya 16 Bora Alhamisi hii. Arsenal walipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa goli moja na BATE ya nchini Belarus, katika mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette alionyeshwa nyekundu dakika ya 85 hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza jijini London usiku wa Alhamisi. 

Nafuu kwa kocha Unai Emery ni kurejea kwa mshambuliaji Pierre Emerick Aubameyang ambaye aliukosa mchezo wa kwanza kwa ugonjwa. Pengine alhamisi tutamshuhudia Mesut Ozil akipewa nafasi ya kucheza baada ya mashabiki wengi wa klabu hiyo kulalamikia Ozil kuachwa nje ya kikosi licha ya kuwa yuko fiti kucheza. Mechi hii itaonyeshwa Mubashara kupitia chaneli ya ST World Football pekee majira ya  saa 2:55 Usiku Alhamisi.

Kwa upande wa Chelsea wao wanatarajia kufuzu kufuatia ushindi wa magoli 2-1 waliupata ugenini dhidi ya Malmo FF Alhamisi ya wiki iliyopita katika mchezo wa kwanza. Licha ya kupoteza dhidi ya Manchester United siku ya Jumatatu Chelsea watatarajia kupumzisha baadhi ya wachezaji ili kuwaweka fiti kwa ajili ya mechi ya fainali ya Kombe la ligi, Uingereza siku ya Jumapili.

Mchezo wa Chelsea dhidi ya Malmo FF utapigwa majira ya saa 5:00 Usiku Alhamisi na utakuwa LIVE kupitia chaneli ya ST World Football pekee.
Michezo mingine itayakayochezwa Alhamisi Usiku Saa 2:55 ni Villareal vs Sporting CP (Sports Premium), Eintrancht Frankfurt vs Shakhtar Donetsk (Sports Focus) na ile ya Saa 5:00 Usiku ni SL Benfica vs Galatasaray (Sports Focus), Bayer Leverkusen vs FC Krasnodar (Sports Arena), Inter Milan vs SK Rapid Wien (Sports Premium) na nyingine zote kupitia chaneli za michezo sa StarTimes.

Michezo yote ya Europa league inaonekana kupitia StarTimes ambapo mteja anatakiwa kulipia kifurushi cha kati, kwa upande wa Antenna ni MAMBO Tsh 14,000 pekee na kwa upande wa dish ni SMART kwa Tsh 21,000 pekee. Pia mechi za Arsenal na Chelsea zina uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...