Na Agness Francis, Blogu ya Jamii. 
Kampuni ya Blockbonds yenye makao makuu yake nchini Norway kwa kushirikiana na Benki ya I & M ya Tanzania  wamezindua rasmi huduma mpya  bunifu ijulikanayo kwa jina la SPENN yenyekuweza kufanya malipo bure ya kutuma na kutoa hela. 

Huduma hiyo bunifu itapatikana kupitia Benki ya I &M  itakayokuwezesha kufanya miamala mbali mbali  bure, ambapo utaweza kufungua akaunti binafsi na ya biashara kiganjani mwako. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo  Afisa Mtendaji  Mkuu wa Blockbonds na SPENN  Jens Glaso Jijini Dar es Salaam ameeleza kuwa anafuraha kubwa kuingiza rasmi huduma hiyo katika soko lingine barani Afrika baada ya kufanikisha kuizindua  rasmi nchini Rwanda mnamo Mwaka jana ambayo mpaka sasa inawatumiaji zaidi ya 130,000  nchini humo. 

"Ni rahisi sana mtu yoyote anayemiliki  simu aina ya Smartphone  (simu janja)  anaweza kujisajili na huduma ya SPENN  Kwa urahisi ambapo ili kujisajili unapaswa kuwa na namba ya simu, jina kamili pamoja na namba ya kitambulisho cha Taifa kinachotolewa na NIDA"amesema bwana Glaso. 

Aidha mkurugenzi mtendaji  Benki ya I&M  Baseer Mohammed  amesema kuwa benki hiyo imejikita   zaidi katika huduma za kidigitali na SPENN ambayo huduma hiyo inalenga kukidhi mahitaji na matarajio ya wateja  wake. 

"Huduma hiyo inayobadilisha namna ambavyo watanzania wanafanya miamala yao ya kifedha na kufanya mfumo mzima wa kufanya miamala kuwa na ufanisi zaidi, wenye usalama na pasipo kuwa na gharama, vilevile tunaamini kabisa huduma ya SPENN  itachangia katika kuboresha maisha ya Watanzania "amesema Baseer Mohammed. 

Hata hivyo Meneja masoko na mawasiliano Benki ya I & M Emmanuel Kiondo amesema kuwa sababu ya kutimia simu janja kupakua App ya SPENN  na kufanya miamala yote iliyotajwa wamezingatia sababu za kiusalama zaidi.
Afisa Mtendaji  Mkuu wa Blockbonds na SPENN  Jens Glaso  akizungumza wakati wa uzinduzi huo   kuhusu huduma hiyo ya SPENN inavyoweza kufanya kazi na kurahisisha kufanya kazi kwa kuondoa mfumo wa uchumi unaohitaji fedha taslimu kufanya miamala  Jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi mtendaji  Benki ya I&M  Baseer Mohammed akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam kuwa Benki ya I &M imejikita zaidi katika huduma za kidigitali na SPENN ikiwa  malengo yao ni kukidhi matarajio ya Wateja.
.Wadau mbalimbali waliojitokeza katika uzinduzi huo wa huduma ya SPENN kwa kushirikiana na benki ya I & M   Jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...