Kocha
Mkuu wa timu ya KMC ya Manispaa ya Kinondoni, Etiene Ndayiragije akiwa pamoja na Mchezaji
wa timu ya Alliance FC yenye maskani yake jijini Mwanza Tanzania,
Dickson Ambundo.
Kocha
Mkuu wa timu ya KMC ya Manispaa ya Kinondoni, Etiene Ndayiragije,
akionyesha furaha baada kupokea tuzo ya Bikosports Tanzania, kufuatia
kuwa kocha kocha bora wa mwezi Januari, ambapo Kampuni ya BikoSports
waendeshaji wa mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani
ndio wadhamini wa tuzo hiyo waliobarikiwa na Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF). Picha na Mpigapicha Wetu.
Mchezaji
wa timu ya Alliance FC yenye maskani yake jijini Mwanza Tanzania,
Dickson Ambundo, akiwa mwenye shangwe nyingi baada ya kupokea tuzo ya
mchezaji bora wa mwezi January kutoka kwa Msemaji wa Bikosports, Geofrey
Lea, waendeshaji wa mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali
duniani ambao ndio wadhamini wa tuzo hiyo waliobarikiwa na Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
WAENDESHAJI
wa mchezo wa kubashiri matokeo wa Bikosports, jana wamewakabidhi tuzo
zao, Etiene Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya KMC ya Kinondoni jijini
Dar es Salaam na mchezaji wa Alliance FC ya jijini Mwanza, Dickson
Ambundo, baada ya kuibuka kocha bora na mchezaji bora wa mwezi January.
Makabidhiano
ya tuzo hizo yalifanyika Makao Makuu ya Bikosports jijini Dar es
Salaam, huku tuzo hizo zikiwa na lengo mahususi la kuongeza ari katika
harakati za kukuza na kuendesha mpira wa miguu nchini Tanzania.
Akizungumzia
tuzo hiyo, Kocha wa KMC, Etiene Ndayiragije, aliwashukuru Bikosports
kwa kuamua kuingia kwenye tuzo hizo akiamini kuwa kwa pamoja
zitafanikisha sekta ya mpira wa miguu kupiga hatua kubwa.
"Nawashukuru
walioniona kwamba nastahili kuwa kocha bora wa mwezi January, huku tuzo
hii nikiamini nimeipata kwa sababu ya sapoti kubwa ninayoipata kutoka
kwa wachezaji wangu wote pamja na uongozi wangu wa KMC," Alisema
Ndayiragije.
Naye
Ambundo aliyeibuka kwenye Mchezaji Bora wa mwezi January, alisema kwa
kupata tuzo ya Bikosports anaamini ataongeza bidii kubwa katika safari
yake ya mpira wa miguu, jambo ambalo limechangiwa na nguvu kubwa
anayoiweka katika timu yao ya Alliance yenye ndoto kubwa ya kufanya
vizuri.
"Nadhani
nimestahili kabisa kuitwaa tuzo hii na ninaamini kuwa naweza kuipata
tena kwa sababu lengo langu ni kucheza mpira mzuri na kuisaidia timu
yangu ya Alliance, hivyo ninachofanya ni kuongeza nguvu katika
kumsikiliza mwalimu wangu, kuishi vizuri na wachezaji wenzangu ili wote
tufikie malengo yetu," Alisema Ambundo.
Akizungumzia
tuzo hiyo, Msemaji wa Bikosports, Geofrey Lea alisema kuanzisha tuzo
hiyo ni sehemu ya kuhakikisha kwamba mpira unakuwa kwa kiasi kikubwa,
huku wakiomba ushirikiano mkubwa kutoka kwa wadau wa mpira wa miguu
wakiwamo wanaobashiri matokeo kwa kupitia kampuni yao ya Bikosports.
"Hii
ni safari nzuri ya kukuza mpira wa miguu hivyo wadau wote kwa pamoja
tunaomba ushirikiano wao, ambapo katika nyanja ya ubashiri wa matokeo,
Bikosports
ndio Kampuni inayotoa zawadi kwa haraka huku jamvi lao likiwa ni rahisi
kushinda kuliko michezo yoyote Tanzania, ambapo namba ya Kampuni ni
101010, huku mchezaji akiweza kubashiri kwa simu ndogo kwa namba
*149*89# au wanaobashiri kwa mtandao https://www.bikosports.co.tz/ ambao ni rahisi kucheza na kushinda pia," Alisema Jeff Lea.
Kuanzishwa
kwa tuzo ya Bikosports kwa kocha bora na mchezaji bora ni sehemu muhimu
ya kuhakikisha kwamba wachezaji na makocha wao wanaongeza bidii kubwa
katika kuhakikisha kwamba wanapata maendeleo makubwa ndani ya uwanja,
ambapo mbali na tuzo hizo, pia huambatana na Sh Milioni moja.
mwisho
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...