Na Munir Shemweta,  BUCHOSA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula  ametoa hati za ardhi kwa wananchi kumi na tisa wa halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza na kuifagilia halmashauri hiyo kwa  kuwa na mfumo mzuri wa kutunza kumbukumbu za majalada ya ardhi.

Dkt Mabula alitoa pongezi hizo leo tarehe 15 Februari 2019 alipozungumza na wananchi wa Buchosa wakati wa kukabidhi hati za ardhi  akiwa katika ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli yaserikali kupitia kodi ya ardhi.

Alisema,kwa mara ya kwanza katika ziara zake kwenye halmashauri mbalimbali  ameikuta halmashauri ya Buchosa ikiwa inatunza kumbukumbu za majalada ya ardhi kwa mujibu wa sheria sambamba kuwepo mawasiliano kati ya afisa mmoja kwenda kwa mwingine wakati wa kushughulikia majalada na kuongeza kuwa migogoro mingi ya ardhi inayojitokeza inasababishwa na utunzaji mbaya wa majalada ya ardhi.

"Taratibu za utunzaji majalada ya ardhi pamoja na mawasiliano baina ya ofisa mmoja na mwingine zimekaa vizuri ni tofauti kabisa na niliyoyaona katika halmashauri nyingine,  Buchosa mko vizuri" alisema Dkt Mabula.

Alizungumzia utoaji hati kwa wananchi wa Buchosa,  Dkt Mabula aliwapongeza wananchi hao kwa kupatiwa hati na kueleza kuwa wananchi hao wanaelewa kuwa ardhi ni mali na hati walizokabidhiwa zitawawezesha kukuwa kiuchumi.

Alisema, mambo makubwa yanayofanyika nchini kama ununuzi wa ndege,  mradi wa treni ya mwendokasi, mradi wa kufufua umeme wa  Stiglers George ni jitihada za serikali ya awamu ya tano katika kuwahudumia wananchi na hayo yote yatafanikiwa kwa wananchi kutekeleza jukumu la kulipa kodi ikiwemo ile ya ardhi.

Aliongeza kwa kusema  wananchi 19 waliopewa hati watafungua milango kwa wananchi wa Buchosa na wengine kuchangamkia kupata hati ambapo pengine walikuwa hawajui kama hati inaweza kupatikana Buchosa na kuongeza kuwa wale wananchi walio katika urasimishaji  nao wachangamkie kupata hati. 

Hata hivyo, Dkt Mabula pamoja na kuipongeza halmahauri ya Buchosa lakini ameilaumu kwa kushindwa kupanga mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji na kuiagiza halmashauri hiyo kuanza kupanga na kupima pamoja na kuanisha maeneo ya huduma.

 Awali,Afisa Ardhi Mteule Halmashauri ya Buchosa Rafael Kilumanga alisema halmashauri hiyo imepima jumla ya viwanja 886 katika maeneo tofauti ya halmashauri hiyo na viwanja 31 kati ya vilivyopimwa 31 vimemishamilikishwa kwa wananchi  na kutolewa hati.
 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akimpatia hati ya kumiliki ardhi mkazi wa Buchosa mkoani Mwanza Esta Bukombe wakati wa ziara ya kuhamasisha ukusanyaji maduhuli ya Serikali kupitia kodi ya ardhi. (picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi)
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula akikagua mafaili katika  masijala ya ardhi ya Halmashauri ya Buchosa, kushoto ni Afisa Ardhi Mteule Rafael Kilumanga. (picha na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...