NA TIGANYA VINCENT,TABORA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameziagiza wadau wa zao la tumbaku kuhakikisha wanatumia teknolojia ya kisasa na mabani ya kisasa katika kukaushaji wa tumbaku.

Hatua itasaidia kuepusha uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji wa miti mikubwa kwa ajili ya ukaushaji wa tumbaku kwa kutumia mabani ya kizamani.

Makamu wa Rais alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa TASAF wilayani Sikonge ikiwa ni siku tatu ya ziara yake mkoani Tabora .

Alisema miti inayokatwa kwa ajili ya matumizi ya ukaushaji wa tumbaku kwa kutumia katika ukaushaji wa zao hilo ina thamani kubwa kuliko faida wanayopata kutokana na mauzo ya zao hilo.

Makamu wa Rais alisema mauzo ambayo mtu angepata kutokana na uuzaji wa miti ule ule ambao umetumika kuchomea tumbaku ni makubwa kuliko yake ambayo anayapata kupitia uchomeaji tumbaku.

Alisema ni vema wadau wakahakikisha wanashirikiana na Mwekezaji ambaye ameonyesha nia ya kuwekeza katika matumuzi ya teknolojia inayotokana na mwanga jua (solar) na umeme wakati wa kukausha tumbaku ili kupunguza ukataji wa miti kwa ajili ya kupata nishati ya ukaushaji wa zao.

Aidha Makamu wa Rais aliwaagiza wadau wa tumbaku wanapowapokea wanunuzi wa zao hilo wahakikishe wanaweka kipengele cha upandaji miti na utunzaji wa mazingira kabla ya kuingia nao mkataba.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema kuwa ipo haja ya hatua za makusudi zikachukuliwa kuhakikisha kilimo cha zao la tumbaku haliendelei kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira kwa ajili ya kuukoa Mkoa huo kugeuka Jangwa.

Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) Hassan Wakasuvi alimuomba Makamu wa Rais, Ofisi yake isaidie katika ujenzi wa mabani ya kisasa yanayotumia nishati ya jua na umeme wakati wa ukaushaji wa tumbaku katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema katika andiko ambao baadhi ya wadau watakwenda nalo China kwa ajili ya kutafuta masoko zaidi ya zao hilo wamependekeza wanunuzi wanunue tumbaku iliyozalishwa na umeme na mwanga wa jua(solar).

Wakasuvi alisema kwa hali ya wakulima walio wengi hivi sasa wanatumia kuni na hivyo matumizi ya teknolojia hiyo mpya hawawezi kumudu bila kupata msaada wa ujenzi wa teknolojia hiyo mpya.

Katika hatua nyingine Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameziagiza halmashauri nchini kuhakikisha mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato yake ya ndani kwa ajili vikundi inakuwa na tija na sio kama ilivyo sasa.

Hatua itavisaidia vikundi kupata fedha ambazo zitaviwezesha kutekeleza miradi yenye tija kwa wanavikundi na kuwawezesha kurejesha.

Makamu wa Rais alilazika kutoa kauli hiyo baada ya kutoa mkopo wa milioni 40 kwa vikundi 11 vya Halmashauri ya Sikonge.

Alisema kwa kiasi hicho kwa watani wa idadi ya vikundi , kila kikundi kitapata wastani wa milioni 3 ambazo ni kiasi kidogo kwa ajili ya shughuli zao.

Makamu alisema ni vema Halmashauri zinapotoa mikopo zihakikishe kuwa fedha wanatoa katika vikundi zitaleta matokeo mazuri na zitakuwa endelevu kwa ajili ya kuwaendeleza wao na hatimaye kuzirejesha ili ziwasaidie wengine.

Makamu wa Rais aliongeza kuwa Halmashauri hiyo inaweza kuanza na vikundi vichache kwa kuviwezesha ununuzi wa mizinga na ununuzi wa ng’ombe wa kisasa kwa ajili ya kuanzisha ranchi ambao watawasaidia wakopaji kuuzia viwanda malighafi badala ya kuwapa fedha kidogo ambazo haziwasaidii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...