Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema vituo vya afya 350 vitakuwa vimekamilika nchi nzima ndani ya miaka mitano ya Uongozi wa Awamu ya tano

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati alipotembelea kituo cha afya cha Sokoine wilayani ya Singida mkoa wa Singida ikiwa muendelezo wa ziara yake ya kikazi ambapo amekuwa akikagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo.

“Kulikuwa na hospitali 65 za wilaya lakini tulivyoingia madarakani zimejengwa hospitali 67 na lengo kuu ni kuwapa wananchi huduma bora ya afya” alisema Makamu wa Rais.

Aidha Makamu wa Rais alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitokubalina na misaada ya masharti na imejidhatiti kufanya miradi ya maendeleo kwa kutumia fedha zake za ndani.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alizindua barabara ya Karume ambayo inajumuisha mradi wa mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 6.1 ambazo nibarabara ya Karume yenyewe , Boma Kinyeto, Double Road Junction (Semali Singida-Dodoma ).

Sambamba na hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea kituo cha afya Migori ambapo alijionea maendeleo ya ujenzi ambao unatazamiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi machi, pia alitembelea shule ya sekondari ya Mwanamema Shein ambapo alizungumza na wanafunzi na kujionea maendeleo ya ujenzi wa bweni la wanafunzi pamoja na kupanda mti wa kumbukumbu.

Wakati huo huo Naibu Waziri wa maji ameahidi kutoa tanki la maji la lita 10,000 kwa ajili ya kituo cha afya cha Karume ikiwa kama jitihada za kumuunga mkono Makamu wa Rais ambaye amejitoa kuhakikisha afya ya mama na mtoto inakuwa salama.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Migori wilayani Singida kutoka kwa Kaimu Mhandisi wa Wilaya Dayness Rwehumbiza. Kituo cha afya cha Migori ni moja ya vituo vilivyopata shilingi milioni 400 za kitanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimia na Mkuu wa Sule ya Sekondari ya Mwanamema Shein Bi. Zainab Mtindu wakati akiwasili kwenye shule hiyo iliyopo Migori, wilayani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori wilayani Singida wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yupo ziarani mkoani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Awesu akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori, Singida ambapo aliwasihi wasome kwa bidii ili waje kuwa viongozi bora.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka udongo kwenye mti wa kumbukumbu alioupanda katika shule ya sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori wilayani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Naibu Waziri Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa barbara ya Karume iliyopo Singida mjini ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ndio alikuwa mgeni rasmi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa barbara ya Karume iliyopo Singida mjini. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi  kwenye  ufunguzi wa barabara ya Karume iliyopo Singida mjini. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...