Na Ripota  Wetu.

WANAMGAMBO wa itikadi kali wanaojiita "Dola la kiislam"-IS wamejaribu kuiokoa ngome yao ya mwisho mashariki mwa Syria huku wake na watoto wao wakiyapa kisogo mapigano makali katika eneo hilo.

Vikosi vya wanamgambo wa kiarabu na kikurdi vinavyopigania kidemokrasi nchini Syria, SDF vimeanzisha opereshini kubwa jumamosi iliyopita kwa lengo la kuwatimua wapiganaji wa dola la kiislam , IS au Daesh kutoka ngome yao ya mwisho miongoni mwa ngome walizokuwa wakizizidhibiti tangu mwaka 2014 nchini Syria na Iraq.

Maelfu ya watu wamekuwa wakikimbia mnamo siku za hivi karibuni kutoka kile kinachojulikana kama eneo la Baghouz", karibu na mpaka wa Iraq, wengi wao ni wanawake na watoto, ingawa wanamgambo wa itikadi kali pia ni miongoni mwao.

Taarifa ya Mwandishi Hamidou Oummilkheir/AFP ambayo imehaririwa na Iddi Ssessanga imesema kuwa tangu Desemba mwaka jana zaidi ya watu 38, 000, wengi wao wake na watoto wa wapiganaji wa itikadi kali wameyakimbia maeneo yaliyokuwa yakishikiliwa na IS.

"Tumevikomboa vituo kadhaa vilivyokuwa hapo awali vikidhibitiwa na IS". msemaji wa vikosi vinavyopigania demokrasi nchini Syria, SDF, Mustafa Bali amesema.Shirika la Syria linalosimamia masuala ya haki za binadamu limesema wanamgambo wanaoungwa mkono na Marekani wanasonga mbele kidogo kidogo. 

"Miripuko imetegwa kila mahala katika eneo hilo" amesema kiongozi wa shirika hilo lenye makao yake nchini Uingereza, Rami Abdul Rahman.Vikosi vinavyopigania demokrasia nchini Syria SDF vimeanzisha opereshini ya kijeshi kuwatimua wapiganaji wa itikadi kali wa Is toka mkoa tajiri kwa mafuta wa Deir Ezzor tangu Septemba mwaka jana na kwamba tangu wakati huo zaidi ya wapiganaji 1300 wa SDF na wanajihadi 650 wameuliwa huku raia zaidi ya 400 wakipoteza pia maisha yao.

Rais Donald Trump wa Marekani aliashiria uwezekano kwa vikosi vya muungano kutangaza ushindi mnamo siku chache zinazokuja dhidi ya IS. Ushindi wa vikosi hivyo katika kijiji cha Baghouz utaiwezesha Marekani kuwahamisha wanajeshi wake 2000 kutoka Syria, kama alivyotangaza rais Trump decemba mwaka jana.

"Tunaambatana na wakati ili kuweza kuheshimu ahadi tuliyotoa" amesema kaimu waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan alipokuwa ziarani nchini Iraq jana bila ya kutaja lini hasa wanajeshi wa Marekani wataondolewa Syria. CHANZO DW .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...