Aliyekuwa Makamu  wa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Michael Wambura akiwa katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri Kusomewa mashtaka yake ya yanayomkabili. Wambura anadaiwa kuwa na mashtaka zaidi ya kumi
 Aliyekuwa Makamu  wa Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF), Michael Wambura akimsikiliza wakili wake, wakati akiwa katika viunga vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akisubiri Kusomewa mashtaka yake ya yanayomkabili.
Na Karama Kenyunko globu ya Jamii. 

Aliyekuwa makamu wa rais wa Shirikisho la  mpira wa miguu nchini (TFF), Michael Wambura amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 17 yakiwemo ya kutakatisha fedha.

Katika kesi hiyo mshtakiwa wambura anakabiliwa na shtaka moja la kughushi, Shtaka moja la kutoa nyaraka za uongo, mashtaka 13 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na mashtaka mawili ya kutakatisha fedha.

Akisoma hati ya mashtaka wakili wa serikali George Barasa akisaidiana na  Moza Kasubi pamoja na Imani Mitumezizi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina imedaiwa mshtakiwa alitenda kosa la kughushi Julai 6,2004 mahali pasipojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam. 

Imedaiwa siku ya tukio mshtakiwa Wambura kwa nia ya kutapeli  alitengeneza barua ya  kughushi ambayo haina kumbu kumbu namba akionyesha  imeandikwa na E Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa  kampuni ya Jeck system anadai kurejeshewa malipo ya mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba aliyokuwa ameikopesha TFF.

Katika shtaka la kutoa Nyaraka ya uongo imedaiwa, mshtakiwa  alitoa barua iliyokuwa haina kumbu kumbu namba  ya tarehe 6/7/2004 akijifanya kwamba ni barua iliyoandikwa na Maganga ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Jeck system ltd. akidai kuwa  anadai mkopo wa USD 30,000 pamoja na riba waliokopeshwa TFF huku akijua kuwa siyo kweli.

Aidha katika shtaka la 3 hadi la 15 mshtakiwa anadaiwa kujipatia kiasi jumla ya zaidi ya sh. Milioni 95 
 kwa njia ya udanganyifu akidai kuwa fedha hizo ni sehemu ya malipo ya jumla ya kiasi cha fedha mbali mbali na riba kutoka kwa Jek huku akijua kuwa siyo kweli.

 Katika moja ya mashtaka hayo ya kujipatia fedh kwa njia ya udanganyifu imedaiwa, Juni 17.2015 huko katika ofisi za TFF kwa njia ya udanganyifu, Wambura alijipayia sh. Milioni 10 kutoka TFF kwa kuonesha kuwa ni malipo ya USD 30,000 pamoja na riba kutoka kwenye kampuni hiyo ha Jeck jambo ambalo siyo kweli.

Katika mashtaka ya utakatishaji fedha imedaiwa, kati ya Agosti 15 na Oktoba 21 huko katika ofisi za TFF mshtakiwa alijipatia sh. Milioni 25,050,000   kutoka TFF huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la kughushi.

Pia imedaiwa kati ya Machi 16 na Oktoba 21 2015 mshtakiwa alijipatia sh. Milioni 75,947,924 kutoka TFF wakati akijua fedha hizo siyo halali zimetokana na shtaka la kughushi.
Hata hivyo. Mshtakiwa hakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa kesi hiyo imefunguliwa chini ya sheria ya uhujumu uchumi ambapo mahakama ya Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika
Baada ya upande wa mashtaka kumaliza kumsomea wambura mashtaka yake, wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo kwa sababu mashtaka yote 17 hakuna shtaka hata moja lilolofunguliwa chini umya sheria ya uhujumi uchumi hivyo yalitakiwa yafunguliwe kama mashtaka ya kesi ya kawaida ya jinai ambayo yanamruhusu mshtakiwa kujibu.

Kufuatia hoja hiyo, Hakimu Mhina ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 14 kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi, Wambura amerudishwa rumande.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...