Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange akipokea Dhana za kufundishia Masuala ya Familia na Malezi ya Mtoto kutoka kwa Mkurugenzi  Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Idara ya Watoto Sehemu Familia na Malezi Bi. Grace Mwangwa   wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.
 Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange akikabidhi Dhana za kufundishia Masuala ya Familia na Malezi kwa Afisa Maendeleo ya Jamii aliyewakilisha Mkoa wa Shinyanga wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto. 
 Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Simon Anange akiongea na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Katavi wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.
 Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto wakiwa katika kazi ya vikundi kujadiliana namna bora ya kuwasiligsha mafunzo hayo kwa Jamii kabla ya kufungwa kwa mafunzo hayo mapema leo Katika mji mdogo wa Kasulu. 
Mkurugenzi  Msaidizi Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Idara ya Watoto Sehemu Familia na Malezi Bi. Grace Mwangwa akiongea na Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa ustawi wa Jamii   wakati wa kufunga mafunzo kwa maafisa hao kuhusu mafunzo ya uelimishaji Jamii  kwa kutumia Kitini cha Familia na Malezi ya Mtoto.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma Kanali Simon Anange amesikitishwa na watoto kufanyiwa vitendo vya ukatili na ndugu na watu walioaminiwa kuwalea au kuwatunza iwe nje au manyumbani kwao.
Akifunga Mafunzo ya siku nne kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii pamoja na Maafisa Ustawi wa Jamii kuhusu matumizi ya Kitini cha Malezi ya Mtoto na Familia yalitolewa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendelep ya Jamii  Kanali Anange amesema amesema asilimia 40 ya vitendo vya ukatili inafanyika mashuleni ikiwemo utani wa kumdhalilisha mtu na kufanya watoto kuichukia shule.
Akiutaja unaofanyika mashuleni Kanali Anange amesema ni ukatili wa kunyanyasa mtu kwa kumtania jambo ambalo limechangia baadhi ya watoto wanaokumbwa na kadhia hiyo kugoma kwenda shule.
Aidha Mkuu wa Wilaya hiyo amelitaja tatizo la kibinafsi kuwa linachangiwa na wazazi wa siku hizi kuwalea watoto katika mazingira ya kujitenga tofauti na hapo awali ambapo mtoto kimsingi alikuwa ni mtoto wa Jamii nzima.
Amesema tatizo tulilonalo la watoto wa mitaani linatokana na malezi mabaya kwani katika Jamii ya watu wa Zanzibar hakuna watoto wa mitaani akiitaja Tanzania bara kukosa upendo kwani Jamii yetu inayojiita imeendelea imezidisha ubinafsi kwa kuwa na upendo tu kwa watoto walio wazaa tu bila kuangalia watoto wengine walipokosa upendo na kukimbilia mitaani.
Ameitaja jamii kuanagalia kile tunachokiita kuendelea kama kinaleta tija kwani maendeleo ya sasa ya mtoto kula katika saani peke yake kinamfanya kufikili kuwa cha kwake ni cha kwake matokeo yake ni kuwa na jamii yenye ubinafsi na maendeleo ya sasa yanakiuka misingi muhimu kama zamani kwa kisingizio cha maendeleo na kuongeza kuwa wakati mwingine maendeleo ya sasa yanaipeleka jamii kuendekeza mambo yasiyokuwa ya razima.
Wakati huohuo Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Familia kutoka Wizara ya Afya, Idara  Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Grace Mwangwa amesema ili kuweza kuendeleza Jamii zetu Serikali kupitia Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto imejipanga kutokomeza mila mbaya katika Jamii na kuenzi mila nzuri lakini pia kuitaka jamii kutambua kuwa kuna tofauti kati ya kutunza na kulea watoto.
Aidha Bi. Mwangwa amesema kuwa Serikali imejiwekea malengo kupitia mpango kazi huo kuwa ifikapo mwaka 2022 serikali iwe imetokomeza vitendo vya ukatili katika Jamii na kuongeza kuwa mpango huu pia unaangalia mazingira salama ya mtoto akiwa shuleni lakini pia katika Jamii.
Mafunzo haya kuhusiana na malezi ya mtoto na familia yamefanyika kwa wataalamu wa maendeleo ya Jamii kutoka Mikoa ya Shinyanga, Kigoma na Katavi na mikoa hii kwa kiasi kikubwa ina changamoto ya uwapo wa mimba na ndoa za utotoni lakini yanafanyika huku Taifa likuwa linakumbwa na kitisho kipya cha mauaji ya watoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...