Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nchini kutoka Wizara ya Afya, Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii  Neema Mwanga ametoa onya kuwa atachukua hatua kali dhidi ya Shirika lolote Lisilo la Kiserikali litalokiuka kufanya kazi kwa mujibu wa matakwa ya Sheria ya NGOs ya Mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005.
Akiwa katika ziara ya kutembelea mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyoko katika Mkoa wa Kilimanjaro Msajili Mwanga amesema kuwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanawajibu wa kuzingatia kanuni mpya za Sheria ya NGOs zinazoelekeza Mashirika hayo kufanya kazi kwa kuzingatia Misingi ya uwazi na uwajibikaji maana miradi hiyo imeanzishwa kwa lengo la kuwanufaisha wananchi ambao ndio walengwa wakuu.
Msajili Mwanga aliwaambia viongozi wa Mashirika manne aliyoyatembelea leo hii ikiwemo TAWREF, White Orange, Elimu Mwangaza na Tusonge Community Organisation kwamba Misingi ya uwazi na uwajibikaji kama inavyobainishwa katika Sheria hiyo inasisitizwa kwa lengo la kukuza ushiriki wa wanufaika katika kutambua vyanzo vya mapato ya NGOs, kiasi cha fedha zinazopolkelewa na mashirika na kutoa taarifa za miradi yao inayotekelezwa kwenye ngazi ya jamii ili kufuata matakwa ya kisheria na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Kufuatia azma ya Serikali ya kuacha kufanya shughuli za NGO kwa mazoea, Msajili Mwanga ameonya kuwa NGO yoyote itakayobainika kufanya kazi bila kusajiliwa au kupata hati ya ukubalifu itakosa sifa na kupelekea kupata zuio la usajili kwa mujibu wa kanuni ya sheria ya NGO ya mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005.
‘’Naelekeza NGO zote kubainisha kazi zinazotekelezwa, kwa sasa tuko kwenye hatua ya kuwajengea wadau wote wa NGOs uelewa ili kuwezesha kila mmoja kuzingatia sheria na mashirika amabyo yatashindwa kuzingatia sheia, taratibu na kanuni za utekelezaji wa miradi yao zitashurutishwa kusitisha miradi yao maana hazitakuwa na sifa stahiki”. Alisema Msajili  N. Mwanga.
Katika ziara hiyo ya kikazi Msajili wa NGOs amepongeza kazi inayofanywa na Mashirika ya TAWREF, White Orange, Elimu Mwangaza na Tusonge Community Organisation na kuwataka Wakurugenzi wa taasisi hizo kwa kuzingatia vipaumbele vya Mikoa, Halmashauri, na changamoto zinazowakabili wananachi katika Mkoa wa Kilimanjaro na nje ya Mkoa huo. Ameongeza kuwa utendaji wa Taasisi hizo umeonesha kuzingatia yale yaliyobainishwa katika kanuni za sheria ya NGOs na kuwataka kuwasiliana na Ofisi ya Msajili ngazi ya Taifa, Mkoa na Halmashauri katika kuendelea kuboresha mazingira ya kazi zao kama kutakuwa na suala lenye kuwatatiza katika utendaji wa akzi zao. 
Aidha Msajili Mwanga amewataarifu wadau wa NGOs kuwa katika kuhakikisha Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanatatuliwa chanagmoto zinazowakabili, Serikali Inaendelea kukamilisha mfumo wa usajili na utoaji wa taarifa kwa njia ya mtandao (online). Mfumo huu utatumiwa na wadau, wasajili wasaidizi ngazi ya mikoa na Halmashauri pamoja na Ofisi ya Msajili ya taifa. Juhudi hizi zitasaidia Taifa kukuza mchango wa Mashirika katika uchumu wa Taifa na kukuza uwajibikaji.
Wakati huo huo Mkurugenzi wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nchini Neema Mwanga amebainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya Idara kuu ya Maendeleo ya Jmaii Jinsia wazee na watoto inakamilisha kanzidata ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali hapa Nchini ili kuwa na nyenzo ya kufuatilia mchango wa mashirika hayo katika pato la Taifa. Wakti huo huo Ofisi ya Msajili wa NGOs inaandaa mfumo wa Ufuatiliaji na tathmini ili kufanikiha kazi ya uratibu kwa kuonesha wadau kutambua maungufu yao na kuyafanyia maboresho katika muda stahiki. Juhudi hizi zitasaidia mfumo wa uratibu katika ngazi mablimbali kuwa na uelewa wa pamoja na kuchukua hatua dhidi ya Taasisi ambayo itaonekana kutozingatia sheria.
Wakiongea kwa muda tofauti wakati wa ziara hiyo Bw. Michael Reuben ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ‘Elimu Mwangaza’ amepongeza juhudi za Wizara katika kutatua chanagmto zinazokwamisha ufanisi katika utendaji wa NGOs Nchini. Moja ya hatua iliyofurahiwa na wadau wengi ni uandaaji wa mfumo wa usajili kwa njia ya matandao ili kupunguza gharama za safari wakati wa kufuata huduma hiyo.
Vilevile mmoja wa viongozi wa NGOs moja kutoka Manispaa ya Moshi(jina limehifadhiwa) ameeleza ziara ya Msajili amabye amefika katika Ofisi ya Shirika hilo imekuwa na manufaa makubwa maana imemjengea ari na uelewa wa kukamilisha taratibu za uasajili ili atambuliwe na hivyo kuendesha kazi zake kwa mujibu wa matakwa ya kisheria. 
Mwisho Neema amepongeza Maafisa Wasaidizi wa Mkao wa Kilimanjaro kwa namana wanavyotekelezakazi yao ya kusimamia na kuratibu kazi za NGos kwa weledi katika uzingatiaji wa kanuni za sheria ya NGOs ya Mwaka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2005. Watendaji hao wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri wamekumbushwa wajibu wao wa kuyasimamia Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa  kufuata katiba, Sera za kitaifa, kanuni za maadili, vipaumbele vya kijamii, vibali vya kazi kwa watendaji wasio raia wa Tanzania pamoja na umuhimu wa uwasilishaji wa mikataba ya miradi ya kazi zilizopata ufadhili kwa ajili ya utekelezaji.
Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yanadhamana ya kutoa mchango katika jamii masikini na isiyo na uwezo ili kuwezeshwa katika kuboresha ustawi na maendeleo ya maisha ya wananchi wenye uhitaji. 
Katikati Katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha S. Amour na Katibu Tawala wa Msaidizi Utawala Bwai Biseko wakifuatilia kwa makini maelezo ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Nchini wa (pili kulia) Neema Mwanga na ujumbe wake kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa ziara ya kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika mkoa huo.
Kulia, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Moshi Bw. Michael Mwandezi akiongea na Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali wakati  Neema Mwanga  kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati wa ziara ya kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika mkoa wa Kilimanjaro.
Msajili wa Mashirika Yasiyo Yakiserikali Neema Mwanga(kulia) kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akipokea maelezo ya shughuli za Mradi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Lisilo la Kiserikali la ElIMU MWANGAZA Bw. Michael Reuben liloko Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa ziara ya kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika mkoa huo .
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la TAWREF, Dafrosa Itemba (kushoto)akitoa ufafanuzi wa mafanikio ya Shirika hilo kwa Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Neema Mwanga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Msajili huyo kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika mkoa wa Kilimanjaro mapema wiki hii.
Msajili wa Mashirika Yasiyo Yakiserikali Bi. Neema Mwanga (Katikati) kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akisisitiza hoja ya kisheria ya uwazi na uwajibikaji kwa uongozi wa Shirika Lisilo la Kiserikali la TAWREF (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kufuatilia uratibu na usajili wa NGOs katika Mkoa wa Kilimanjaro mapema wiki hii. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...