Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Evaristo Longopa akifungua mafunzo ya Uelewa Juu ya Usimamizi wa Viashiria Haratishi ( Risk Management) kwa Wakuu wa Divisheni na Vitengo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.Mafunzo hayo ya siku tatu na ambayo yatakuwa shirikishi yataiwezesha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kuandaa Mwongozo wake wa Usimamizi wa Viasharia Hatarishi. Mwongozo ambao utaendana na majukumu na mazingira ya Ofisi.



Na Mwandishi Maalum, Dodoma 

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeandaa mafunzo ya uelewa juu ya usimamizi wa viashiria hatarishi kwa watumishi wake ( Risk Management) 

Mafunzo hayo yanayotolewa na Mwezeshaji kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani Bw. Onesmo Mbekange yatafayika kwa siku tatu, na yamefunguliwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Evaristo Longopa. 

Akifungua mafunzo hayo siku ya jumanne, yaliyoanza na Wakuu wa Divisheni na Vitengo katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Dk. Longopa amesema, mafunzo hayo ni muhimu sana kwa yatasaidia na kuboresha utendaji na utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu. 

Dk. Longopa vilevile ameyataja mafunzo hayo kuwa , yatawezesha watumishi wote kuwa na uelewa wa pamoja wa viashiria hatarishi ambavyo kama havitathibitiwa mapema vinaweza kukwamisha kufikiwa wa malengo ambayo Ofisi imejiwekea. 

Akasema , hapana shaka, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu kama ilivyo kwa Taasisi nyingine, ina viashiria vingi vya hatari na hivyo kuwataka watumishi wote kuhakikisha wanayatumia mafunzo hayo kujijengea uelewa ili kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Naibu Mwanasheria Mkuu amewaeleza wakuu hao wa divisheni na vitengo kwamba, baada ya mafunzo hayo ambayo yatakuwa shirikishi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali itakamilisha mchakato wa kuandaa Mwongozo wa Usimamizi wa Viashiria Hatarishi ( Risk Management Framework). 

Katika mafunzo hayo, Bw. Onesmo Mbekange, ameeleza kuwa kila Wizara na Taasisi za Serikali bila la kujali ukubwa au udogo wake zinapashwa kuwa na Mwongozo wa namna ya kukabiliana na viashiria hatarishi vinavyotokana na utekelezaji wa majumu yao ya kitaasisi au ki-wizara. 

Akasisitiza kuwa endapo Taasisi inakuwa tayari na mfumo au mwongozo wa usimamizi wa viashiria hatarishi, unaipa mwanga na utayari Taasisi wa nini kitatokea na namna gani ya kukabiliana na hatari hizo kabla hazijatokea. 

“Ukiwa na Mwongozo kunaiwezesha Menejimenti ya Taasisi kufanya maamuzi sahihi na mapema kabla ya tukio halijatokea badala ya kusubiri mpaka tatizo litokee” Amesema Bw.Mbekange. 

Aidha amebainisha kwamba, Mwongozo wa Usimamizi wa Viashiria Hatarishi pia unaiwezesha Taasisi kufikia malengo ambayo Taasisi imejiwekea, na gharama ndogo na utendaji wa Taasisi unaimarika. 

Ameeleza zaidi kwamba, Wizara au Taasisi za Serikali kutokuwa na Mwongozo huo, pamoja na mambo mengine kunapelekea ukiukwaji na kutokuzingatiwa kwa sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa. 

Mwaka 2012 Wizara ya Fedha na Mipango iliandaa Mwongoao wa Kitaifa wa Maandalizi na Usimamizi wa Vihatarishi na kuagiza Wizara na Taasisi za Serikali kuandaa Miongozi itakayotekeleza agizo hilo. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikali 
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...