RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  ameungana pamoja na Wapiganaji wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama waliovyoshiriki katika Maadhimisho ya sherehe za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika chakula maalum cha mchana alichowaandalia.

Chakula hicho maalum cha mchana aliwaandalia kutokana na ushiriki wao kwenye sherehe hizo za miaka 55 ya Mapinduzi zilizofanyika Januari 12 mwaka huu 2019 huko katika uwanja wa Gombani Chake Chake Pemba.

Hafla hiyo ya chakula maalum ilifanyika leo katika  Kambi ya Mafunzo ya Jeshi ya Chukwani ambayo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mawaziri, Manaibu Mawaziri na viongozi wengine pamoja na Wapiganaji wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika shukurani zake Dk. Shein kwa Wapiganaji hao zilizotolewa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu alitoa pongezi kwa Wapiganaji hao kwa kushiriki kikamilifu katika sherehe hizo adhimu.

Alieleza kuwa hatua hiyo ya Dk. Shein ya kuwaandalia chakula maalum cha mchana ni utamaduni aliouweka kila mwaka baada ya kumaliza sherehe hizo ambayo inaonesha wazi jinsi alivyokuwa na upendo pamoja na imani kubwa na wananchi wote anaowaongoza.

Hivyo,  Waziri Gavu alisisitiza haja kwa Vikosi hivyo vya Ulinzi na Usalama kuendelea kutimiza wajibu wao wa kulinda amani, utulivu na mshikamano ambapo pia, alitumia fursa hiyo kutoa pongezi maalum kwa ushiriki wao mzuri katika sherehe hizo.

Waziri Gavu alitoa shukurani za dhati kwa vikosi hivyo kwa kuazimisha kwa hali ya juu kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.

Waziri Gavu alisema kuwa gwaride hilo lililovutia sana lilikuwa ni kielelezo cha kutosha cha Mapinduzi ya Januari 12.1964 yaliyowakomboa Wazanzibari wote ambayo yataendelea kulindwa, kuenziwa na kutunzwa daima.

“ Imani ya kiongozi mwema siku zote haitafutwi kwenye jarida bali inatafutwa katika nafsi na nyonyo za watu anaowaongoza........na sote tunaona jinsi ya upendo ulionao kwa wananchi wa Zanzibar na Tanznia nzima kwa jumla”.

“ .....hongereni sana sana sana Vikosi vyetu vya Ulinzi na Usalama kwa kazi kubwa mliyoifanya katika kilele cha miaka 55 ya Mapinduzi yetu ”,alisisitiza Waziri Gavu.

Aidha, alitoa shukurani kwa Wapiganaji wote pamoja na viongozi wao kwa kufanikisha kilele cha sherehe hizo na kusisitiza haja kwa vikosi hivyo kuendelea kusimamia amani, utulivu na mshikamano hatua ambayo itawapelekea viongozi wengine kutekeleza majukumu yao ya kuwaletea maendeleo wananchi kwa ufanisi mkubwa.

Nae Kaimu Brigedi Kamanda 101 KV Zanzibar Kanal Salum Serengo Mugoba alitoa shukurani na pongezi kwa Dk. Shein kwa kuendelea kuvijali vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na kuendeleza utamaduni wake huo aliouweka kwa kila mwaka mara baada ya sherehe za Mapinduzi ambapo Dk. Shein huwandalia chakula maalum cha mchana Wapiganaji hao na kula nao pamoja.

Kanal Mugoba alieleza kufarajika kwao na hatua hiyo ya Dk. Shein na kutoa pongezi na shukurani kwa niaba ya Wapiganaji wote walioshiri katika hafla hiyo adhimu.

Ni utamaduni aliouweka Dk. Shein wa kuwaandalia chakula cha mchana Vikosi vya Ulinzi vinavyoshiriki katika gwaride la sherehe za Mapinduzi pamoja na vijana na Wanafunzi ambao hushiriki sherehe hizo kwa kila mwaka ambapo hapo jana aliwaandalia vijana na Wanafunzi  chakula hicho huko katika Makao Makuu ya KVZ, Mtoni mjini Zanzibar.

Katika hafla hiyo pia, Kikundi cha Taarab cha Taifa kilitumbuiza pamoja na Grassbanda ya JWTZ.


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali.S.S.Mugoba, alipowasili katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika Uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba mwaka huu 2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama wakati ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika viwanja vya Kambi ya JWTZ Chukwani Zanzibar, kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mikoa na Idara Maalum za SMZ.Mhe. Haji Omar Kheri.(Picha na Ikulu) 
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa amesimama, ukipigwa wimbo wa Taifa baada ya kuwasili katika Viwanja vya Kambi ya Chukwani kujumuika na Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama kujumuika katika chakula maalum aliowaandalia kushoto Kaimu Kamanda wa Brigedi ya 101KV Zanzibar, Kanali S.S.Mugoba na kulia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ. Mhe. Haji Omar Kheri,(Picha na Ikulu)
 KAIMU Kamanda Brigedi ya 101 KV Zanzibar Kanali S.S.Mugoba, akizungumza wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Aki Mohamed Shein, kwa ajili ya Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi zilizofanyika mwaka huu kisiwani Pemba January,12, 2019.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akijumuika katika chakula maalum aliowaandalia, Askari wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama, katika kambi ya chukwani  walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu zilizofanyika Kisiwani Pemba katika uwanja wa gombani.
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama walioshiriki Gwaride la Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi Zanzibar, wakijumuika katika hafla ya chakula maalum walioandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika Kambi ya Chukwani Zanzibar.
 ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakijumuika katika hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.
 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Kambi ya Chukwani Zanzibar.
ASKARI wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu akitowa shukrani kwa niaba ya Rais wa Zanzibar, wakati wa hafla ya chakula maalum kilichoandaliwa kwa ajili yao katika kambi ya Chukwani Zanzibar.(Picha na Ikulu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...