Addis Ababa, 7 February 2019.

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika nafasi yake ya mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End Malaria Council) jana aliendesha kikao cha kikazi na wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Africa. Katika Kikao hicho Mhe. Kikwete alielezea umuhimu wa kuwekeza nguvu za pamoja katika kuutokomeza ugonjwa wa malaria katika bara letu la Afrika. 

Katika Mwaka 2017. Malaria iliua watu 435,000 duniani, wengi wao wakiwa ni watoto. Asilimia tisini ya vifo hivyo vilitokea Africa. Pamoja na kuwa kumekuwa na juhudi kubwa za kutokomeza malaria, Ugonjwa huo umeendelea kuwa tishio kubwa katika juhudi za maendeleo. Ni katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo, Mhe. Kikwete na taasisi ya kutokomeza malaria imeonelea ishirikiane na shirikisho hizo za kikanda kuwa na mikakati ya pamoja katika kutokomeza malaria.

Mhe. Kikwete aliitambulisha rasmi taasisi hiyo ya kutokomeza malaria kwa wajumbe. Taasisi hiyo iliyoanzishwa na Bill Gates pamoja na Ray Chambers kwa kushirikiana na taasisi ya wadau wa malaria inayojulikana kama Roll Back Malaria Partnership to end Malaria inajumuisha viongozi wenye nguvu za ushawishi na pia watu wenye uwezo wa kifedha ambao huziwekesha kwenye shughuli za maendeleo. 

 Wajumbe kwenye taasisi hiyo ni Bill Gates, Ray Chambers .Peter Chernin, Aliko Dangote, Mhe.Jakaya Kikwete, Graça Machel, Luis Alberto Moreno, Mhe. Ellen Johnson Sirleaf, na mwenyekiti wa ALMA ambaye kwa kipindi hiki ni Mfalme Mswati III wa Ufalme wa Eswatini.

Ikumbukwe kuwa Mhe. Kikwete ni mkereketwa mkubwa katika masuala ya Afya. Katika kipindi chake cha urais aliweza kushirikisha maraisi wa Afrika kupambana na malaria kupitia chombo alichokianzisha kinachojulikana kama African Leaders Malaria Alliance (ALMA). Katika kikao hicho Katibu Mkuu wa secretariat ya chombo hicho alimshukuru Mhe. Kikwete kwa kuanzisha chombo hicho ambacho kilianza na marais nane na sasa kinajumuisha marais wote wa Africa. 

 Naye Katibu Mkuu wa SADC Dr. Stergomena Tax, alisema taasisi yake ipo tayari kufanya kazi na Mhe. Kikwete na taasisi ya kutokomeza malaria, kwani kwa SADC suala la malaria limepewa kipaumbele kikubwa. Wajumbe wote waliokuwapo katika kikao hicho wakiwemo wawakilishi wa umoja wa Afrika na RBM walimpongeza mhe. 

Kikwete kwa uongozi wake katika masuala ya malaria na kuelezea utayari wao wa kufanya kazi pamoja naye na na taasisi ya kutokomeza malaria. 
 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika nafasi yake ya mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End Malaria Council) (wa pili kulia)  jana akiendesha kikao kazi cha wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Africa. Katika Kikao hicho Mhe. Kikwete alielezea umuhimu wa kuwekeza nguvu za pamoja katika kuutokomeza ugonjwa wa malaria katika bara letu la Afrika. 
 Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete katika nafasi yake ya mjumbe wa taasisi ya kutokomeza malaria (End Malaria Council) jana akiendesha kikao kazi cha wakuu mbalimbali wa Shirikisho za Kikanda za Kiuchumi za Africa. Katika Kikao hicho Mhe. Kikwete alielezea umuhimu wa kuwekeza nguvu za pamoja katika kuutokomeza ugonjwa wa malaria katika bara letu la Afrika. 

 Picha ya pamoja 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...