Rais wa Sudan Omar al-Bashir ametangaza hali ya hatari nchini humu na kufutilia mbali utawala wa majimbo na uongozi wake.

Katika hotuba yake kwa taifa rais Bashir alisema kuwa maandamano yanayoshuhudiwa nchini yanalenga kuvuruga amani na kuhujumu utawala wake.

"Natangaza hali ya hatari kwote nchini kwa mwaka mmoja."

"Natangaza kuvunjiliwa mbali kwa utawala wa majimbo katika ngazi zote hadi za mikoa."

Waandamanaji walimiminika katika mji wa Omdurman baada ya tangazo hilo, lakini waliyoshuhudia wanasema maandamano hayo yalizimwa na polisi kwa kutumia bomu ya machozi.

Saa kadhaa baada ya tangazo hilo rais Bashir amewateua wakuu wa vikosi vya usalama kuchukua nafasi ya magavana waliyofutwa kazi.

Katika hotuba yake kwa taifa bwana Bashir ameliomba bunge kuahirisha mchakato wa marekebisho ya katiba ambao ungemruhusu kugombe muhula mwingine madarakani.

Bashir pia alisema kuwa maandamano yanayoshuhudiwa nchini yanalenga kuvuruga amani na kuhujumu utawala wake.

Ripoti za awali kutoka shirika la kitaifa la ujasusi (NISS) ziliashiria kuwa Bashir huenda akajiuzulu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...