Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema ni marufuku mtu yeyote tofauti na Rais Dk. John Magufuli kujiita Rais au kiongozi yeyote kuingilia madaraka ya mwingine katika mkoa huo na kwamba kufanya hivyo ni kinyume cha Katiba, sheria na taratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari Chalamila amesema upo mtindo wa baadhi ya wabunge kujiita marais na kwamba kufanya hivyo ni kosa kwani mbunge hawezi kuwa Rais na wala hawezi kufanya majukumu ya Rais.

Anasema ni vyema watu wajitambue na kila kiongozi kumiliki majukumu yake pasipo kuingilia nafasi au mhimili mwingine wa dola ili kuepusha migongano na mifarakano katika utendaji kazi wao.

“Nimesema watu wajitambue, ni marufuku wewe mbunge kujiita Rais kwasababu Rais ni Mhimili mwingine. Ni marufuku mimi mkuu wa mkoa kujiita Mbunge, ni marufuku mtendaji wa mtaa kujiita mtendaji wa kata au wa kata kujiita wa mtaa, kila mtu amiliki majukumu yake,” anasema na kusisitiza.

“Rais ni mmoja wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hatuna Rais mwingine labda wale ambao wanaandikwa kwa R ndogo na narudia tena Rais hawezi kuwa Mbunge na wala Mbunge hawezi kuwa Rais.

Anasema inashangaza sana kuona mtu kutoka mhimili mmoja wa dola anakwenda kuingilia mhimili mwingine na kwamba kujiita jina la mwingine si haki.Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa alisema licha ya kwamba mkoa huo umetawaliwa na viongozi wa upinzani hususan Halmashauri ya Mbeya mjini lakini wamekuwa wakishirikiana vizuri na serikali katika utendaji kazi.

Anasema linapokuja suala la utekelezaji wa mambo ya maendeleo baraza la madiwani limekuwa likiweka kando itikadio zao za vyama na kuwa kitu kimoja kupigania maslahi ya Taifa.

“Mkoa wetu hauna misigano kutokana na siasa, madiwani wanashirikiana vizuri na serikali na serikali imekuwa ikishirikana vizuri na madiwani katika kutekeleza miradi ya maendeleo bila kujali chama gani kinatawala katika eneo fulani ndiyo maana serikali ilipeleka Sh bilioni 700 katika kata ya Mzavua kwaajili ya ujenzi wa kituo cha afya licha ya kuwa kata hiyo ipo chini ya diwani wa Chadema ambaye ndiye Meya,” anasema Chalamila.

Anasema madiwani hao ndio waliopitisha uamuzi wazo lakela kuhamisha Sh milioni 300 kutoka shule ya Mkapa kwenda shule ya Azimo na kwamba kama kusengekuwa na ushirikiano wangeweza kugoma kupitisha wazo hilo.Hata hivyo alisema ipo haja ya wananchi kuendelea kuelimishwa na kuona kuwa serikali inapeleka maendeleo kwa wananchi si kwasababu ya vyama vyao.

Aliongeza kuwa katika kipindi alichofanya kazi katika mkoa huo amesimamia mambo mbalimbali ikiwemo ulinzi na usalama na kuondoa sifa mbaya ya mkoa huo kuwa mkoa wa mauji.Anasema mkoa huo umeendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato, uboreshaji wa elimu na kuongeza ufaulu pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya afya, barabara na maji
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, akiwa katika Mahojiano Maalum na vyombo vitatu vya habari jijini Dar es Salaam 
Baadhi ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mahojiano na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila jijini Dar es Salaam

--

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...