Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imesema kuwa kumekuwa na ushirikiano na Sekta ya Umma katika kwenda katika soko ikiwa ni kuondoa changamoto zilizokuwa zinawakabili sekta hiyo.

Akizungumza na waandishi habari Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Geofrey Simbeye amesema serikali imekuwa na utayari wa kukutana na kujadiliana na sekta binafsi kwa kuonyesha nia madhubuti ya kuboresha mazingira ya Uwekezaji nchini.

Amesema kuwa spidi ya serikali ya awamu tano ya Rais Dk. John Magufuli nchi itafikia soko kwa kuongeza Kampuni hadi kufikia milioni moja.

Simbeye amesema kuwa mkutano waliokuwa waufanye jijini Dar es Salaam wameiahirisha kutokana na washiriki kuwa wengi na kuamua kufanya katika kanda kwa nchi nzima.

Aidha amesema miundombinu mbalimbali inayojengwa watautumia ni sekta binafsi katika kurahisisha mazingira ya kufanya biashara.

Amesema sekta binafsi inazidi kuimarika kutokana na mazungumzo ya mara kwa mara na serikali ikiwa ni kuondoa vikwazo vya kibiashara na serikali imekuwa na uwazi katika kufanya utatuzi wa vikwazo hivyo.

Simbeye amesema kufanya majukwaa katika kanda ni kuweka uwigo mpana wa kila mdau kushiriki kuliko ingefanyika sehemu moja ambayo kwa idadi ya isingetosha.

"Serikali imedhamiria kushirikana na TPSF na mafanikio yameanza kuonekana na sio kukosoa kila kitu ina haki ya kupongezwa"amesema Simbeye.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Geofrey Simbeye akizungumza na waandishi habari kuhusiana na mwitikio wa serikali katika utatuzi wa changamoto za biashara pamoja na mkutano uliotakiwa kufanyika Dar es Salaam sasa kufanyika katika kanda zote nchini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...