Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Simba wamefanikiwa kushinda bap 1-0 katika mchezo wao wa Kundi D dhidi ya National Al Ahly ya Misri katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. 

Mchezo huo ulioanza kwa kasi katika dakika 10 za Kipindi Cha kwanza kwa timu hizo  kusomana na kushambulia kwa kupokezana.

Katika kipindi cha kwanza Simba walishindwa kutumia nafasi walizozipata ingawa walifanikiwa kupata kona kwa wingi. Dakika 45 za Kipindi cha kwanza kilimalizika timu zote zikienda mapumziko wakiwa wako 0-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Al Ahly wakilisakama lango la Simba, lakini umakini wa safu ya ulinzi ya Simba iliweza kuondoa mipira kwenye lango lao. Dakika ya 65, mchezaji wa Kimataifa kutoka Rwanda Meddie Kagere aliipatia Simba goli la kwanza akipokea pasi ya Zana Coulibaly baada ya kuwahadaa ngome  ya Al ahly.

Mpira uliendelea kwa kasi Simba wakilinda goli lao na kutafuta goli lingine zaidi huku Al ahly wakisaka la kusawazisha. Mpaka mpira unamalizika katika Uwanja wa Taifa Simba wanafanikiwa kuondoka na alama tatu, na kutimiza alama 6 akiwa nyuma ya Al Ahly mwenye alama 7 na nafasi ya tatu akiwa As Vita na alama 4 huku JS Saoura akiwa na alama 2.

Katika mchezo mwingine wa kundi D As Vita anakaribishwa ugnini dhidi JS Saoura mechi itakayochezwa majira ya saa 4 usiku kwa saa zaAfrika Mashariki.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...