Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mchezo wa Kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Singida United na Coastal Union sasa kufanyika Jijini Dar es Salaam. Singida United wameuomba uongozi wa TFF kuuruhusu mchezo huo kuchezwa Jijini Dar badala ya Singida kutokana na ugumu wa ratiba ya ligi na FA.

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United United Festo Sanga amesema kuwa Kutokana na Ugumu wa ratiba yetu ya Ligi na kombe la FA, Mchezo wao dhidi ya Costal Union wa kombe la FA sasa utachezwa Dar es Salaaam tar 23/02/2019 badala ya Namfua Singida  ulivyopangwa awali.

Amesema kuwa,  leo Jumatano wanacheza na Ndanda Fc huko Mtwara, hivyo kesho  timu inatakiwa iondoke Mtwara kurejea Singida ambapo kwa umbali wa Mtwara hadi Singida ni safari ya Siku mbili, hivyo timu ingefika Singida tarehe Februari 22.

Sanga ameeleza kuwa mechi yao dhidi ya Coastal itachezwa Feb  23 wakiwa nyumbani Namfua na wameona kuwa  Jambo hilo tumeona sio salama kwa Afya ya wachezaji na mchezo husika.

Ameeleza kuwa kwa pamoja  viongozi wa Singida United wameuomba uongozi wa TFF ambao wao ndiyo wanaosimamia kombe la Azam Sports Federation Cup (FA) watubadilishie Uwanja ili kuendana na muda, angalau timu ipumzike na iweze kucheza Feb 23.

Sanga amewashukuru  TFF kwa kukubali ombi lao na wamewapatia Uwanja wa Azam Complex  na mechi itachezwa saa 1:00 usiku.

Uongozi wa Singida United umewaomba radhi kwa mashabiki na wanasingida, kwakuwa wameamua kubadili uwanja na wamefanya hivi kwa afya ya wachezaji wao na mchezo wenyewe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...