SMARTLAB imeamua kuunda mfumo maalumu ambao utawakutanisha vijana kwa lengo kuwajengea uwezo utakaowawezesha kufanya shughuli mbalimbali za ujenzi wa uchumi wao binafsi na Taifa kwa ujumla.

Miongoni mwa mambo ambayo vijana hao wanafundishwa na kuelekezwa ni katika mambo ya ujasirisamali, ubunifu wa kibiashara, kubuni miradi, kutafuta masoko na kuangalia namna ya masoko ya Tanzania yanavyoweza kutumika kuuza bidhaa zinazozalishwa nchini.

Akizungumza leo Februari 8, 2019 Meneja Mradi wa Smartlab Juliana Kayombo amesema kuwa miongoni mwa vijana ambao wamewakutanisha wamo pia  wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini ambapo kwa pamoja wanatumia nafasi hiyo kujeanga uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali.

Amefafanua Smartlab hii ni mara ya tatu kupitia mradi wake wa kuwaunganisha vijana na kupitia Smartlab Founder to Founda wameweza kukutanisha vijana wengi na wapo ambao wamenufaika kwani wapo ambao wameweza kuanzisha kampuni zao na wengine wamefanikiwa kujiajiri na msingi wake ni baada ya kukutana na kupeana maarifa.

“Kupitia Smartlab vijana wa kada mbalimbali wanakutana na kujadiliana mambo mengi yanayohusu ujasiriamali, ubunifu , utafutaji masoko, uwezeshaji na namna ya kutumia fursa zilizopo nchini kuanzisha kampuni,”amesema.

Kwa upande wake Mwanzilishi wa Smartlab ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Smart Codes Limited Edwin Bruno amesema kuwa uwepo wao sasa umetoa nafasi ya vijana kukutana na kujadili mambo ya maendeleo.

“Ukweli ni kwamba sasa vijana wajasiriamali, wabunifu na wavumbuzi wa biashara za hapa nchini wana sehemu moja ya kukutana na kufanya kazi zao ambazo zitakutanisha na kukuza jumuiya za uvumbuzi zilizo tofauti na zenye vipaji hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla,”amesema.

Wakati huo huo Mdhamini Mkuu wa Smartlab kutoka Raha Liquid Telecom Kumeil Abdulrasul amesema wanajivunia kuona kumeanzishwa  sehemu moja ambayo itawakutanisha watu wa kada mbalimbali na hasa vijana kwa lengo la kujengeana uwezo na kupeana maarifa kuhusu nini cha kufanya kuanzisha biashara, kampuni na shughuli nyungine za kiuchumi.

“Tumefurahishwa zaidi na hili eneo la ubunifu , kwetu sisi Raha Liquid Telecom moja ya mambo ambayo tumeyapa kipaumbele ni ubunifu ambao umetusaidia kufanya mambo makubwa.Nchi yetu inahitaji kuona tunakuwa na vijana wengi wabunifu ili tuendelee kusonga mbele kimaendeleo,”amefafanua. 






 Mwanzilishi wa SmartLab na Mkurugenzi Mtendaji wa Smart codes,Edwin Bruno akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu wavumbuzi ,Wajasiriamali na wabunifu wa  Tanzania sasa wana sehemu moja ya kukutana na kufanya shughuli  mbalimbali ili  kukuza jumuiya ya uvumbuzi  hapa Tanzania na Africa  kupitia  Smart codes.
Meneja Mradi wa SmartLab, Juliana Kayombo akiwaeleza waandishi wa habari utekelezaji wa miradi huo.leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi wa SmartLab, Juliana Kayombo (wa pili kulia) akifafanua jambo katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
Mwanzilishi wa SmartLab na Mkurugenzi Mtendaji wa Smart codes,Edwin Bruno  (kulia) akimshukuru  Mdhamini mkuu  kutoka Raha Liquid Telecom,Kumeil Abdulrasul, Bidhaa.
Wajasiriamali,wabunifu na wavumbuzi wakiwa katika mkutano wa kujadili mambo mbalimbali uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...