Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye mkutano maalumu na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019. (Picha zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) akifuatilia kwa makini mkutano maalumu na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akifuatilia kwa makini mkutano maalumu na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) akifuatilia mkutano maalumu na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019.
Walioketi Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Katikati), Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Wa pili kutoka kushoto), Mhe Omary Mgumba (Wa pili kutoka kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe (Kulia), pamoja na Mshauri mwelekezi wa kilimo Prof Marcellina chijoriga wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi za Utafiti katika Sekta ya Kilimo pamoja Watendaji Wakuu wa Sekta Ndogo ya Mazao ya Kilimo uliofanyika ukumbi wa Mvuvi House Jijini Dar es salaam, Leo tarehe 11 Februari 2019.


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) amesema ipo haja ya kuanzishwa kwa Sheria ya Kilimo itakayotoa suluhisho la changamoto zinazamkabili Mkulima na Sekta hiyo kwa ujumla.


Waziri Hasunga ameyasema hayo leo tarehe 11 Februari 2019 wakati wa kikao cha siku mbili baina yake na Watafiti wa kilimo kutoka Taasisi mbalimbali za kilimo nchini.“Kuna kila sababu ya kuanzishwa haraka sheria ya kilimo, kwa sababu hatuna Sheria ya Kilimo na inayotumika sasa ni Sera ya Kilimo, iliyotungwa mwaka 2013 ambayo pia inahitaji kupitiwa upya” amesema

Mhe. Hasunga ameongeza kuwa Sheria zinazotumika kwa sasa ni za Bodi za Mazao mbalimbali, ambazo pia zinachangamoto zake na kuna mazao ambayo hayana Bodi kiasi kwamba kuwatetea Wakulima wa mazao hayo inakuwa vigumu.Mazao yaliyo katika utaratibu wa Bodi ni pamoja na zao la Pamba, Kahawa, Chai, Korosho, Pareto na Tumbaku kwa upande wa mazao ya biashara, mazao ambayo hayana bodi ni yale ya chakula ambayo nayo yana mchango mkubwa katika uchumi wa Taifa.

Waziri Hasunga amewataka Watafiti hao kutumia kikao hicho kutoa michango yenye tija, nini kifanyike katika Sekta ya Kilimo kwakuwa Watafiti wana wigo mpana wa kuitoa Sekta hiyo kutoka sehemu moja hadi nyingine.Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Omary Mgumba alisema kikao hicho ni cha kipekee kwakuwa kimewakutanisha Wataifiti na Wataalamu kutoka Taasisi za utafiti na watafiti wakufunzi wabobevu kutoka vyuo vya kilimo nchini.

“Ni furaha kuwaona leo hii kwa wingi wenu, eneo kubwa la kutiliwa mkazo ni katika suala la masoko, tunafanya tafiti nyingi kuhusu mbegu bora lakini hatuna tafiti za kutosha kuhusu masoko ya mazao ya kilimo,” Alikaririwa Naibu waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...