Na Ripota Wetu
UMOJA wa Afrika umependekeza kufanyika mkutano wa kimataifa Julai mwaka huu kwa ajili ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Libya na pia kuitisha uchaguzi Oktoba.

Katika taarifa yake, umoja huo umesema leo Februari 12 ,2019 mkutano huo utafanyika ili kutafuta maridhiano chini ya uratibu wake pamoja na Umoja wa Mataifa. Pia umeiomba Tume ya Umoja wa Afrika kushirikiana na Umoja wa Mataifa na Serikali ya Libya kwa ajili ya kupanga uchaguzi wa urais na bunge mnamo Oktoba mwaka huu.

Mwenyekiti wa sasa wa Umoja huo, Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi amesisitiza kuwa matatizo ya Afrika yatatatuliwa na waaafrika wenyewe na kwamba Libya imekuwa chini ya tawala hasimu na makundi ya wanamgambo tangu kuuawa kwa Moammer Ghadaffi mwaka 2011.

Inaelezwa kuwa uhasama ni baina ya Serikali inayotambulika na jumuiya ya kimataifa pamoja na ile inayoungwa mkono na Jenerali Khalifa Haftar.

CHANZO: DW

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...