Upelelezi katika kesi ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile inayomkabili msanii Rutyfiya Aboubakary maarufu Kama Amber Rutty na mume wake Said Mtopali umekamilika na sasa kesi hiyo itaanza kuunguruma Machi 7 kwa washtakiwa hao kusomewa maelezo ya awali.

Wakili wa Serikali, Faraji Nguka ameeleza hayo leo Februari 11.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili Nguka amedai, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa lakini upelelezi umekamilika, hivyo wanaomba tarehe kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali. Kufuatia taarifa hiyo,  Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi March 7, 2019. Amber Rutty na mumewe walifikishwa mahakamani hapo November 2, 2018 wakikabiliwa na kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Mbali na wawili hao, mshtakiwa mwingine ni James Charles maarufu kama ‘James Delicious’.

Katika kesi hiyo kosa la kufanya mapenzi kinyume na maumbile linamkabili Amber Ruth, ambapo anadaiwa amelitenda kati ama baada ya October 25, 2018 ambapo alimruhusu Said Bakary kumuingilia kinyume na maumbile, kosa ambalo amelikana.

Pia kosa jingine la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, linamkabili mshtakiwa wa pili Said Bakary ambapo anadaiwa kati ama baada ya October 25,2018 jijini Dar es Salaam alifanya mapenzi na Amber Rutty kinyume na maumbile ambapo alisema si kweli.

Kosa la tatu la kuchapisha video ama picha za ngono, ambapo linamkabili James Charles ama James Delicious akidaiwa kati ya October 25,2018 alisambaza video za ngono kupitia magroup ya Whatsapp.

Kosa jingine la nne ni kusababisha kusambaa picha za ngono linamkabili Amber Ruth na Said Aboubakary ambapo wanadaiwa kati October 25,2018 walisababisha kusambaza picha za ngono kupitia makundi ya Whatsapp. Kosa ambalo wamesema si kweli.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...