Anaandika Abdullatif Yunus – Kagera

Ni Tarehe 08, Februari, 2019 usiku vilio, simanzi na hofu vinatawala katika mtaa wa Hamugembe, Nyangoye Manispaa ya Bukoba Eneo maarufu sana kwa matukio ya ajali mbalimbali zilizogharimu maisha ya watu na wengine kufariki kabisa.

Usiku huu tena ikiwa yapata majira ya saa tatu usiku, unasikika mshindo mkubwa wa Ajali ukihusisha Magari mawili yaliyogongana uso kwa uso, magari hayo ni Roli dogo aina ya Canter,yenye namba za usajili T223 ATK mali ya Bwana Jibril, pamoja na Gari dogo la Abiria Daladala yenye namba za usajili T 869 CHT, inayofanya safari zake Kutoka Bukoba kwenda Mutukula. 

Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo Bwana Abdul Itembwe anaeleza kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea katikati ya mteremko wa Nyangoye, ambapo daladala ilikuwa ikipanda na Canter ikiteremka, hivyo gari hiyo aina ya canter kupata itilafu upande wa breki, na kupelekea kuigonga daladala na kuserereka nayo hadi kandoni mwa barabara yapata mita 150 kutoka barabani katikati. 

Hali hiyo ikamkumba na mwendesha pikipiki aliyefahamika kwa jina moja tu Bonge mkazi wa Nyakanyasi, ambae bado haijafahamika alikuwa katika mwelekeo gani. Kufuatia magari hiyo kugongana mara baada ya kuwa tayari yamesimama, zilianza kuibuka cheche ndogo ndogo upande wa daladala wakati jitihada za uokoaji zikiendelea kujaribu kuwanasua marehemu wa ajali hiyo.

Shuhuda huyo anaongeza kuwa ghafla moto mkubwa ulilipuka na kuanza kuunguza gari hilo huku ndani wakionekana watu watatu ndani ya Daladala, ambao walionekana kupoteza fahamu kama sio kufariki kabisa. Wakati hayo yakiendelea tayari upande wa gari aina ya Roli ambalo lilikuwa na abiria wawili pamoja na dereva, abiria hao walifanikiwa kunusurika na kutoka kupitia dirisha la mlango wa abiria kabla gari halijashika moto .

Wakati jitihada za uokoaji zikiendelea inadaiwa kuwa dereva wa Roli Marehemu Dickson Ndyetabula (25) alijitahidi kujinasua lakini haikuwa rahisi huku akipiga ukulele mkubwa wa kuomba msaaada, licha ya wasamaria mwema kufika eneo hilo na kuanza kumvuta, lakini alionekana kukwama na hivyo hadi mauti yanamkuta alisikika akisema “…Asanteni kwa msaada wenu mimi nakufa..” hadi Jeshi la Polisi na lile Uokoaji (zimamoto) wanafika eneo la tukio tayari moto ulishawazidia wananchi ambao awali walionyesha juhudi za kuuzima kwa maji na mchanga ikiashindikana.

Usiyoyafahamu kuhusu Madereva wote wawili: marehemu Nelsoni Nestory Gerevazi (Miaka 32), Dereva wa Daladala iliyoungua iliyokuwa ikifanya safari za Bukoba – Mutukula, ameacha Mjane na watoto Watatu, ambapo kwa mujibu wa mke wake Bi. Adelina Marchol (34), anasema kuwa mumewe kabla ya mauti kumkuta aliondoka asubuhi kuelekea kazini mara baada ya kupigiwa simu na Tajiri wake (mmiliki wa Hiace) akimtaka aende na Leseni yake, baada ya kupakia na kuondoka kuelekea Mutukula, wakiwa njiani wakirejea walipofika Rwamisheneye ambapo ndipo makazi yao marehemu alimpigia simu Bi. Adelina akimfahamisha kuwa amerejea salama na mizigo alokuja nayo ataileta ngoja kwanza akashushe abiria stendi kuu ya mabasi. 

Baada ya hapo simu aliyoipata nyingine ilikuwa ya Dereva rafiki wa marehemu akimtaarifu habari za ajali na msiba. Kinachoumiza zaidi ni kuwa marehemu Nelsoni katika watoto wake watatu mmoja wa mwisho IVAN NELSON nae ni siku chache zimepita kapata ajali ya Kuungua kwa maji moto wakati akicheza na motto wa jirani na yupo anaugulia nyumbani huku msaada pekee ulikuwa ni baba yake mzazi.

Marehemu Dickson Ndyetabura Jackson (25), yeye ameanza kuendesha magari akitokea katika kazi ya ufundi magari maeneo ya Rwamishenye akiajiriwa na tajili wa kwanza na kuendesha fuso ambalo pia aliliterekeza polini maeneo ya Geita baada ya kuharibika kwa kipindi kirefu, Gari alilopata ajali nalo usiku ni gari amabayo ameanza kuiendesha kwa kipindi cha wiki moja na usiku wa ajali alikuwa akitokea Wilayani Missenyi kuchukua mzigo wa Matikiti maji.

Tayari jeshi la polisi Mkoani Kagera wamethibitisha vifo vya marehemu hao pamoja na marehemu wengine ambao ni pamoja na Peter Ifunya motto wa mwenye Daladala, na Bonge.
Mke  wa Marehemu Bi. Adelina Marchol (34), aliyefariki kwenye ajali hiyo

 Msiba ukiendelea nyumbani kwa marehemu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...