WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka vijana mkoani Kigoma waanzishe mashamba ya michikichi kwa kuwa zao hilo litawapatia kipato cha uhakika. Amesema Serikari imedhamiria kufufua zao la michikichi ili kuliwezesha Taifa kujitosheleza kwenye mafuta ya kula na kuokoa fedha za kigeni.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Februari 18, 2019) alipowasalimia wananchi wa kijiji cha Nyakitondo wilayani Kasulu akiwa njiani kwenda Kibondo.
Waziri Mkuu ambaye yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kufufua kilimo cha michikichi amesema ni vema wananchi wakachangamkia fursa hiyo.

“Vijana limeni michikichi kwani ukipanda ukiwa darasa la tano baada ya miaka mitatu utaanza kuvuna na kujipatia kipato ambacho kitakuwezesha kujikimu.” Amesema kilimo cha zao la michikichi kitawawezesha wananchi hususani vijana kupata mitaji ya uhakika kwa ajili ya shughuli zingine za kiuchumi

Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Tanzania inaongoza kwa kilimo cha zao la michikichi katika nchi za Afrika Mashariki. Kadhalika, Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi hao wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili wawe na uhakika wa matibabu kwa yao na familia zao.
Wakati huohuo Waziri Mkuu ametembelea kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo na kukagua shule ya msingi Kassim Majaliwa na baadae wodi ya wazazi katika Hospitali Nduta.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiingia kwenye moja ya madarasa katika Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa iliyopo kwenye  Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019.  Wapili kushoto ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa Joyce Ndalichako. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua madaftari ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa wakati alipotembelea baadhi ya madarasa ya  Shule hiyo, Februari 18, 2019. Wapili kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa  akiteta na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Profesa, Joyce Ndalichako wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watoto wa Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa  wakati alipokagua madarasa ya Shule hiyo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo, Februari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Kibao kinachoonesha ilipo Shule ya Msingi ya Kassim Majaliwa  katika Kambi ya Wakimbizi ya Nduta wilayani Kibondo ambayo ilitembelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Februari 18, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...