Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru (katikati) akifungua mafunzo ya mfumo wa tathimini na upimaji wa wazi wa utendaji kazi (OPRAS) kwa viongozi wa Hospitali ya Mloganzila.
Baadhi ya viongozi wa hospitali hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji alipokua akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika Februari 19 na Februari 20, 2019 hospitalini hapo.
Mtaalam kutoka Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Renatus Mgusi akiwasilisha mada mbalimbali kuhusu mfumo wa OPRAS.
Dkt. Catherine Shari kutoka Idara ya Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Muhimbili-Mloganzila akichangia hoja katika mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo hayo.


………………………………………


Viongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia Sheria, Kanuni, Maadili na Miongozo ya Utumishi wa Umma ili kutimiza dira na malengo ya Hospitali.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru wakati akifungua mafunzo ya mfumo wa tathimini na upimaji wa wazi wa utendaji kazi (OPRAS) kwa viongozi wa Hospitali ya Mloganzila yaliyofanyika hospitalini hapo.

Akizungumza katika mafunzo hayo Prof. Museru amesema nidhamu na kujituma kwa viongozi kutawawezesha watumishi wa ngazi zote kutimiza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

“Huwezi kufikia malengo yoyote kama hujitumi na kujitoa katika kazi, kiongozi bora ni lazima awe mfano wa kuigwa katika utendaji wake hatua itakayowawezesha watumishi wa chini na wao kufanya kazi kwa bidii”. Amesema Prof. Museru.

Akitoa mada katika mafunzo hayo, mtaalam kutoka Tume ya Utumishi wa Umma Bw. Renatus Mgusi amesema OPRAS ni nyenzo kuu inayotumika katika kutathimini utendaji kazi wa mtumishi hivyo hauna budi kutekelezwa kwa ufanisi.

Mafunzo hayo yatasaidia kuongeza tija na yatawezesha kujiwekea malengo mahususi yanayopimika na yenye uhalisia na ambayo yanawekewa muda maalum wa utekelezaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...