Katibu wa Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Jason Rweikiza(kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu miswada ambayo imejadiliwa bungeni.
Mbunge wa Mbinga Mjini Sixtus Mapunda akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa Sheria ya Vyama vya Siasa
*Wazungumzia umuhimu wa Sheria ya Vyama vya Siasa na faida zake kwa
Watanzania
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
WABUNGE wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) wameazimia kufafanua mambo
mbalimbali ambayo yalijiri katika vikao vya Bunge ambalo limemalizika vikao vyake
Bungeni Mjini Dodoma hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Katibu wa Wabunge hao Jason Rweikiza pamoja na mambo mengine
wamejikita kuzungumzia miswaada sita ambayo imepitishwa na Bunge hilo na
kufafanua kuhusu Sheria ya vya siasa kwa undani zaidi ili umma wa Watanzania
ufahamu kinagaubaga.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Rweikiza amesema wameona ni vema
wakafafanua mambo mbalimbali yakiwemo ya Sheria ya Vyama vya siasa iliyopitishwa kwenye vikao hivyo kwasababu
inaonesha wananchi wengi sio tu hawajahifahamu sawasawa bali pia kuna
upotoshaji mwingi.
"Wabunge wa CCM kwa umoja wetu tumedhamiria kuufahamisha umma kuhusu
mambo ambayo yamejadiliwa bungeni , na hasa miswada sita ambayo imepitishwa
na kuwa sheria.Tanalojukumu la kuhahakikisha Watanzania wanafahamu vema kila
ambacho kimejadiliwa bungeni kwani wabunge tunaotokana na Chama hiki tunayo
dhamana ya kuelezea kwa ufasaha mambo yanavyokwenda,"amesema Rweikiza.
Amefafanua Bunge lilimalizika mwishoni mwa wiki iliyopita lilikuwa mahususi kwa
ajili ya kupokea taarifa mbalimbali kutoka Kamati za Bunge ikiwemo miswada sita
ambayo imepitishwa."Tumekuja kwenu waandishi wa habari tukiamini mtakuwa
daraja la kufikisha haya tunayoyazungumza kwa wananchi."
Akizungumzia zaidi kuhusu Sheria ya Vyama vya Siasa, Mbunge wa Mbinga Mjini
Sixtus Mapunda amesema sheria hiyo ni muhimu kwani sasa Chama cha siasa
ambacho kitaanzishwa kitakuwa kinazingatia maslahi mapana ya nchi yetu badala ya
kuwa chama cha mfukoni au cha kifamilia.
"Ni ukweli usiopinginga kuna vyama hapa vya siasa ambavyo namna
vinavyoendeshwa si kwa ajili ya maslahi mapana ya Watanzania bali ni vyama kwa
ajili ya kunufaisha watu na familia zao.
Hivyo ujio wa Sheria ya Vyama vya Siasa
utasaidida kuweka mambo sawa na kuwa na Chama cha siasa ambacho kitakuwa
kimezingatia mambo yote muhimu ambayo yanatambulika kwa mujibu wa sheria
hiyo,"amesema.
Amefafanua kuwa wameona umuhimu wa kuzungumzia sheria hiyo pamoja na
nyingine kwa kuwa wao ndio wenye Serikali na ndio watakaobeba lawama siku
mambo yakiharibika."Tumekutana nanyi hapa leo hii kufafanua mambo yalijiri
bungeni maana hatutaki kuona wengine wakipotosha, hivyo ni jukumu letu
kuwaambia ukweli ili umma ujue."
Mapunda amesema tangu nchi yetu iingie kwenye mfumo wa Vyama vingi tumefikisha
miaka 26 na katika kipindi chote hicho kuna mambo mengi kama Taifa limejifunza
na hivyo sasa wameamua kuja na Sheria ambayo itaimatisha vyama vya siasa na
hasa kuwa kama taasisi inayoeleweka na sio kuwa na vyama vya siasa ambavyo ni
vya mifukoni.
"Tumeshuhudia malalamiko mengi kutoka kwenye baadhi ya vyama vya siasa ,
kumekuwepo na malalamiko ya matumizi ya fedha.Kuna vyama vya siasa imefikia
mahali Mwenyekiti anakopesha fedha kwa chama.Kupitia Sheria ya Vyama vya Siasa
inakwenda kuweka utaratibu mzuri wa namna gani chama cha siasa kinatakiwa
kuendeshwa,"amesema Mapunda na kuongeza Watanzania wasikubali kupotoshwa
kuhusu sheria hiyo.
Wakati huo huo Mbunge wa Mlalo mkoani Tanga Rashid Shangazi ametumia nafasi
hiyo kuzungumzia hatua ya baadhi ya mapori kupandishwa hadhi na kuwa hifadhi za
Taifa ambapo mbali ya kutunza na kuhifadhi mazingira, ni fursa muhimu kwa
wawekezaji kuwekeza katika hifadhi hizo kwa kujenga hoteli za kitalii.
Ametaja hifadhi hizo ni hifadhi ya Taifa Burigi, Kimisi, Biharamulo, Ibanda na Chief
Rumanyika ambapo amesema pia ni vema TANAPA wakakaa na Mamlaka ya Mapato
Tanzania(TRA) kuangalia namna ya kuangalia namna gani wanaweza kuweka
mazingira mazuri ya msamaha wa kodi kwa baadhi ya vifa kwani TANAPA watakuwa
na jukumu la kujenga miundombinu mbalimbali kwenye hifadhi hiyo.
Pamoja na mambo mengine wabunge hao wa CCM wametoa ufafanuzi kuhusu madai
ya kupotea kwa fedha Sh.trilioni 1.5 ambapo wamefafanua madai hayo hakuna
ukweli wowote bali kuna moja wa Bunge anachokifanya ni kupotosha umma.
Wabunge hao wamesema hata Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali(CAG) imethibitisha hakuna upotevu wa fedha hizo na hivyo
wamewahakikishia Watanzania kupuuza madai ya uwepo wa upotevu wa fedha hizo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...