Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma  imeanza kufanya uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya macho katika kambi maalum iliyoanza tarehe18-2-2019 katika hospitali hiyo na wagonjwa zaidi ya 500 wameshaonwa na mpaka sasa wagonjwa 150 wameshafanyiwa upasuaji na hali zao ni nzuri.

Hayo yalibainishwa na Daktari bingwa wa macho Dk.Frank Sandi wa Hospitali hiyo alipokuwa akizungumzia kuhusu kambi hiyo. "Katika upasuaji wa macho uliofanyika watu wengi waliojitokeza wameonekana kusumbuliwa na matatizo ya mtoto wa jicho na Trakoma kutokana na kuugua mara kwa mara na sababu kubwa ni kutokuosha nyuso zao vizuri”, alisema.

 Dkt. Frank Sandi alisisitiza kuwa tatizo la macho ni kubwa na linatokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuyaweka macho katika hali ya usafi pamoja na kuyakinga na mazingira hatarishi yanayoweza kujeruhi ikiwemo upasauaji wa kuni. “Kati ya wagonjwa waliokuja katibiwa, asilimia 30 ya wagonjwa wamebainika kuwa na ugonjwa wa mtoto wa jicho, na wachache wenye ugonjwa wa vikope (trakoma),”alisema.

 Hata hivyo Dkt Frank alisema kwamba magonjwa mengine yaliyogundulika katika uchunguzi unaoendelea ni pamoja na ugonjwa wa kutoona vizuri na majeraha kwenye macho. “Baadhi ya wagonjwa tuliowaona hapa wameonekana kuwa matatizo ya uoni pamoja na majeraha yanayotokana na kurukiwa na vitu kwenye macho,”alisema. Madhumuni ya kambi hiyo ambayo hufanyika kila mwaka hospitalini hapo kwa kushirikiana na wadau kutoka Marekani ni kutoa huduma za macho kwa wananchi wanaoishi kwenye mazingira ambayo si rahisi kufikika. Na lengo lao mwaka huu ni kuwafikia watu wasiopungua 1,500 na kati yao zaidi ya wagonjwa 400 watafanyiwa upasuaji.

“Hadi sasa tumeshawaona wagonjwa 400 na kati yao, wagonjwa 150 wameshafanyiwa upasuaji. Tunaendelea kutoa huduma za macho kila siku hivyo wananchi wajitokeze kwa wingi kupata huduma hii,” alisema. Naye, Mkazi wa Chimendeli Marta Nhuguti mwenye umri wa miaka 110 aliishukuru hospitali hiyo kwa kutoa huduma hiyo na kudai kuwa alikuwa haoni lakini sasa anaona.
 Madaktari bingwa wa Hospitali ya Benjamin Mkapa na wenzao wa Chuo cha Utah kilichopo Marekani wakifanya uchunguzi na upasuaji wa macho yenye uoni hafifu, mtoto wa jicho na majeraha.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho kutoka Hospitali ya Benjamini Mkapa, Frank Sandi, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye kambi maalum ya tiba kwa wagonjwa wa macho inayofanyika kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho , Frank Sandi akimuonesha   Bi.Martha Nhuguti ishara ya vidole ili kuthibitisha kama anaona vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa macho katika kambi maalum inayofanyika kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Uchunguzi wa macho ukiendelea  katika Hospitali ya Benjamin Mkapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...