Watu wanne wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha magari aina ya Canter lenye namba za usajili T223ATK na Hiace yenye namba za usajili T869 CHC kugongana katika Mlima Nyangoye eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Februari 8,2019.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Revocatus Malimi,ambaye amefika eneo la ajali ambayo imetokea katikati ya barabara,amesema watu wanne wamefariki dunia katika ajali hiyo.

"Canter ilikuwa Main Road ikitokea Rwamishenye ikiingia Mjini kati,baada ya ajali hiyo kutokea,magari hayo yalitoka nje ya barabara,bahati mbaya gari aina ya Hiace ilishika moto na watu waliokuwemo waliungua moto,tumeondoa maiti mbili za abiria na dereva mwenye hiyo Hiace pia dereva wa bodaboda aliyekuwa amefunganishwa kwenye hii ajali bahati mbaya amefariki,kwa hiyo jumla ya watu waliofariki katika ajali hii ni watu wanne,mpaka sasa maiti zipo hospitali ya Mkoa hazijatambuliwa"- RPC

"Bado tunaendelea na shughuli ya uokoaji na uchunguzi kubaini hasa nini chanzo cha ajali hii na atakayebainika kusababisha ajali,hatua za kisheria zitachukuliwa",amesema Kamanda Malimi.



Baadhi ya Wanachi wakitoa msaada wa kuinasua miili ya watu iliokuwa imenasa kwenye magari hayo
Watu wanne wamepoteza maisha katika ajali iliyohusisha magari aina ya Canter lenye namba za usajili T223ATK na Hiace yenye namba za usajili T869 CHC kugongana  uso kwa uso  katika Mlima Nyangoye eneo la Hamugembe Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...