Na Karama Kenyunko Globu ya Jamii. 

* Upande wa utetezi wakieleza  ni wagonjwa

MKURUGENZI Mkuu wa zamani wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu na Astery Ndege ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi na kuisabishia Serikali hasara ya Sh Bilioni 1.16 wameshindwa kufika Mahakamani kwa sababu ni wagonjwa.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),  Leonard Swai ameeleza hayo leo Februari 20.2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo  Salum Ally,  kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya mashahidi (Commital)

Amedai, upande wa mashtaka umepata taarifa kutoka Magereza kuwa washtakiwa wanaumwa, na Leo hawajaweza kufika mahakamani hapo kusikiliza kesi hiyo, ameiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe nyingine, 

Kufuatia taarifa hiyo,  Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 5, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa 

Mbali na Maimu na Kayombo washtakiwa wengine katika kesi hiyo  ni Meneja Biashara wa (NIDA), Aveln Momburi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers,  Astery Ndege, Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond.

Awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 26 likiwemo la uhujumu uchumi,  ila Januari 28,2019 waliachiwa huru na mahakama hiyo baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kusema hana nia ya kuendeleza mashtaka dhidi yao. 

Hata hivyo baada ya washtakiwa kuondolewa mashtaka hayo na kuachiwa huru walikamatwa tena na walifikishwa katika mahakama hiyo kisha kusomewa mashtaka mapya 100 yakiwemo 25 ya utakatishaji fedha.   

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 22 ya kughushi, mashtaka 43 ya kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri, mashtaka mawili ya kula njama, mashtaka 25 ya kutakatisha fedha na mashtaka matano ya kuisababishia hasara NIDA.

Pia washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na shtaka moja la matumizi mabaya ya madara lipo moja ambalo linamkabili  Maimu na Sabina. 

Katika shtaka la kwanza la kula njama, Maimu, Ndege na Ntalima wanadaiwa, kati ya Julai 19, 2011 na Agosti 31,2015 wakiwa maeneo tofauti tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam walikula njama ya kufanya udanganyifu wa Sh.Bilioni 1.175 dhidi ya NIDA.

Pia Maimu anatuhumiwa kutakatisha fedha kiasi cha sh. Bilioni 1,175,785,600.93  kati Julai 19,2011 na Agosti 31, 2015  ambapo anadaiwa kujihusisha moja kwa moja kuhamisha fedha hizo huku akijua ni zao la kosa la kughushi.

Katika shtaka jingine, Maimu na  Raymond wanatuhumiwa Novemba 7, 2011 wakiwa Makao Makuu ya NIDA, Kinondoni jijini Dar es Salama walitumia madaraka yao vibaya na kusababisha  huo cha sheria  (Law School) Dar es Salaam na Kampuni ya Gotham International Ltd kupata faida ya Sh .899,935,494.

Inadaiwa kati ya Novemba 12, 2011 na Mei 12, 2015, Maimu na Momburi wakiwa makao makuu ya NIDA, Kinondoni akiwa Mkurugenzi na Meneja wa biashara walishindwa kusimamia ujenzi wa jengo lililopo plonti namba 39A na kuikuisababishia mamlaka hiyo hasara ya Sh 402,210,885.02.

Katika kesi hiyo washtakiwa, Momburi na Raymond hawakupatikana na kosa la kutakatisha fedha, kwa hiyo mashtaka yao yanadhaminika, ila hadi Mahakama Kuu. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...