Jeshi la Polisi Makao Makuu Kitengo Maalum cha Kupambana na uhalifu kikiongozwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas (pichani), kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe leo tarehe 12/02/2019 limefanikiwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto Mkoa wa Njombe
Kati ya hao watuhumiwa ni pamoja na mhusika wa mauaji ya watoto wa familia moja anayetambulika kwa jina la Joel
Joseph Nziku mwenye umri wa miaka 35 na mkazi wa Magegere, Makambako
Inadaiwa Joel
Joseph Nziku alihusika
na mauaji ya watoto hao siku ya jumamosi tarehe 19.01.2019 majira ya saa moja
jioni, watoto hao ni Godliver Nziku miaka 12, Gasper Nziku
miaka 7 na Giliad miaka 5 wote wakiwa wa familia moja ambao
baba yao alifahamika kwa jina la Danford Nziku miaka 52 mkazi wa kijiji IKando
wilaya ya Makambako mkoani Njombe
Aidha Naibu kamishna Sabas amesema kwa sasa Mkoa wa Njombe na nchi kwa ujumla ni salama na
amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano baina yao na Vyombo vya Ulinzi na
Usalama
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...