Na Said Mwishehe, Blogu ya Jamii
KITUO cha Uwekezaji Tanzania(TIC)kimepokea ujumbe wa watu saba kutoka Hong
Kong -China ambao lengo lake ni kufanya mazungumzo na taasisi mbalimbali za
Serikali na kufanya tafiti kabla ya kuwekeza ikiwemo kwenye eneo la la ujenzi wa
viwanda vya vifaa tiba na dawa.
Akizungumza mbele ya wajumbe hao leo Februari 12, 2019 ,Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu-Uwekezaji Angellah Kairuki amesema ujumbe huo umekuja nchini kwa
lengo la kufanya tafiti katika maeno mbalimbali ya uwekezaji ambapo tangu
wamefika nchini wamekuwa wakifanya mazungumzo na taasisi za Serikali
wakiongozwa na TIC.
"Ujumbe huo kutoka Hong Kong ambayo ni sehemu ya China upo nchini kwa ajili ya
kufanya mazungumzo na taasisi mbalimbali za Serikali.Pia wamekuja kufanya tafiti
na lengo lao kubwa ni kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba,
viwanda vya magodoro pamoja na viwanda vingine kadhaa kulingana na tafiti yao.
"Pia wameonesha nia ya kuwekeza katika kununua ufuta yakiwamo majani yake hasa
kwa kuzingatia ufuta katika nchi hiyo unatumika katika kusaidia pia kutibu
magonjwa mbalimbali na hivyo kiu yao ni kuona wanawasaidia wakulima wa zao hili
nchini Tanzania kuzalisha ufuta kwa wingi.Pia ni fursa ya kupata soko la uhakika
kwani wakulima wetu sasa watakuwa na uhakika wa kuuza majani ya ufuta pamoja
na ufuta wenyewe,"amesema Waziri Kairuki.
Ameongeza pia ujumbe huo baada ya kufika nchini wamefanya mazungumzo na
Bohari ya Dawa nchini(MSD) hasa kwa kuzingatia wanalo eneo la hekari 150 ambalo
wanatafuta watu wa kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.Pia
wamezungumza na uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kuangalia ni namna
gani wawakezaji kutoka Hong Kong wanaweza kuwekeza nchini Tanzania kwa lengo
la kuboresha sekta ya afya.
Waziri Kairuki ameongeza kuwa ujumbe wa watu hao saba , wameonesha nia pia ya
kujenga viwanda vya kuchakata korosho na kwamba kupitia mazungumzo kati ya
ujumbe huo na taasisi za Serikali kuna muelekezo mzuri Hong Kong ambayo
imekuwa na uhusiano mzuri na Tanzania kuwekeza zaidi nchini.Pia amewahakikishia
kuwa Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dk.John Magufuli imeendelea kuweke
mazingira mazuri ya uwekezaji na kwamba ni sehemu salama.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Geofrey Mwambe amesema uhusiano
baina ya Hong Kong na Tanzania umezidi kuimarika katika kufungua fursa za
uwekezaji na utalii na kwamba kihistoria inafahamika Hong Kong ilikuwa ni nchi
inayojitegemea lakini baadae ikawa sehemu ya China.
Amesema kutokana na Hong Kong kuwa sehemu ya China , taarifa nyingi za
uwekezaji ambazo zilikuwa zinatoka Tanzania Hong Kong zilikuwa zinarekodiwa
China, hivyo Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kufanya jitihada ikiwa pamoja na
kufungua Ofisi ya Ubalozi Mdogo ambao kazi yake ni kuimarisha uhusiano wa
kibishara na utalii.
Amesema kuwa Ofisi hizo za Ubalozi Mdogo Hong Kong zinasimamiwa na Balozi
Mdogo Dk.Anne Wu ambaye tangu awali alionesha nia ya dhati ya kuisaidia Tanzania
katika kukuza uhusiano kati yao na Tanzania, hivyo ujumbe wa ujumbe wa watu saba
ni sehemu ya kuimarika kwa uhusiano uliopo.
"Tangu kuwepo kwa Ubalozi Mdogo wa Hong Kong hata idadi ya wanaomba kuja
nchini kwetu imeongeza mara tatu zaidi ya awali.Hata hivyo tunatarajia fursa za
kiuwekezaji na kiutalii kunufaisha sehemu zote mbili.
Watanzania watumie fursa ya
kufanyabiashara Hong Kong na hivyo hivyo Hong Kong nayo itumie fursa hiyo
kuwekeza nchini Tanzania.Tumeendelea kuwahamasisha Hong Kong kuja nchini
kutalii kutokana na vituo vilivyopo hapa kwetu na kweli wameongeza,"amesema
Mwambe na kusisitiza kuwa Tanzania inayo mazingira mazuri ya uwekezaji.
Wakati huo huo Kiongozi wa msafara wa ujumbe huo ambaye pia ni Mwakilishi wa
Balozi Mdogo Hong Kong Dk.Annie Wu, Jessica So amesema ujio wao nchini Tanzania
umekuwa na manufaa makubwa kwani kuna maeneo mengi ambayo yanafaa kwa
uwekezaji na hivyo kupitia utafiti ambao wameufanya kwa kuzungumza na taasisi za
umma kuna maeneo ambayo wameonesha nia ya kuwekeza.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Uwekezaji Angellah Kairuki akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujio wa ujumbe wa watu saba kutoka Hong Kong ambao wapo nchini kuangalia fursa za uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Geofrey Mwambe (aliyesimama) akifafanua jambo leo jijini Dar es Salaam kuhusu ujumbe wa watu saba kutoka Hong Kong ambao wako nchini kuangalia fursa za uwekezaji ukiwemo uwekezaji wa ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...