Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango zinazojengwa katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma. Mpango ameyasema hayo leo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi hizo ambazo zinajengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). 

‘Nafikiri tunaenda vizuri, quality of work inanifurahisha, ikifika tarehe 1 Machi, 2019, nijisikie  nipo huru sasa nabadilisha ofisi nipo Ihumwa’ alisema. Aidha Dkt. Mpango ameuagiza Uongozi wa Wizara kuanza mchakato wa ujenzi wa Jengo kubwa la Ofisi ili kuweza kutosheleza Watumishi wote wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Kwa upande wake Msimamizi wa ujenzi wa Ofisi hizo kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Mhandisi Elisante Ulomi amesema ujenzi wa awamu ya kwanza umejumuisha Ofisi ya Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Manaibu Katibu Wakuu, ukumbi wa mikutano, ofisi za madereva, pamoja na ofisi za Wakurugenzi saba.

Mhandisi Ulomi amesema ujenzi kwa sasa umefikia asilimia 92, na utakamilika tarehe 28 Februari,2019.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isidor Mpango (katikati) akipata maelezo namna ujenzi wa Ofisi za Wizara unavyoendelea kutoka kwa Mhandisi Elisante Olomi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), alipotembelea eneo la ujenzi huo katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isidor Mpango (watatu kulia) akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Bi. Grace Sheshui (wakwanza kulia), wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Khatibu Kazungu, Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isidor Mpango akisaini kitabu cha wageni alipotembelea na kukagua ujenzi wa Ofisi za Wizara hiyo, Ihumwa Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isidor Mpango (kushoto) akioneshwa ramani ya majengo Wizara hiyo kutoka kwa Mhandisi Elisante Olomi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), alipotembelea eneo la ujenzi huo katika Mji wa Serikali Ihumwa Jijini Dodoma. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikali- WFM)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...