Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SERIKALI nchini kupitia Wizara  ya Mifugo  na Uvuvi imewahakikishia wafugaji kuwa hakuna mifugo itakayopotea  kutokana na magonjwa  mbalimbali.

Haya yameelezwa na Naibu  Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdullah Ulega wakati akizungumza na wafugaji wa Wilaya ya Kibaha mkoani  Pwani, wakati wa ziara ya kikazi ya siku moja alioifanya mkoani humo kwa lengo la  kukagua miradi iliyoko chini  ya wizara hiyo.

Amesema Serikali  ilibinafsisha sekta  hiyo  kwa watu binafsi,lakini kwa sasa imerejeshwa serikalini  ili kuwasaidia  wafugaji wa aina zote.

"Kwa sasa  tunazalisha chanjo  ya mdondo zaidi ya milioni 100 kwa mwaka,lengo ni kuwafanya  wafugaji wa kuku na hasa akinamama  waweze kuondokana na umasikini,"amesema Ulega.

Ameongeza  madhumuni ya Serikali ya Awamu ya tano  ni kuhakikisha nchi inakuwa  na mifugo mizuri yenye kuleta tija kwa wafugaji na wawekezaji wa nyama,hivyo amewataka wafugaji kuamini serikali kwa jinsi inavyowapambania katika kuhakikisha soko la bidhaa hiyo  inakuwa kubwa  na yenye tija kwao.

Aidha  ameongeza kuwa kipindi hiki wafugaji nchini wamekuwa  wakinyanyaswa na wafanya biashara kwa kuuza chanjo hizo kwa bei  ya Sh.35,000  mpaka Sh. 45,000 kutokana na hali hiyo Serikali imeamua kusambaza dawa  hizo za chanjo kwa bei ya Sh.20,000, hivyo itawasaidia watanzania  wengi na kuondoa vifo  vya  mifugo.  

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa wlWakala maabara ya vetenari Tanzania,Dk. Furaha Mramba  amesema chanjo zinazozalishwa katika maabara hiyo zinaubora uliothibitishwa na mamlaka za maabara za Mifugo Africa na itakapokamilika itatosheleza mahitaji ya ndani  na nyingine kuuzwa nje ya nchini.

Katika ziara hiyo  Ulega pia ametembelea chamba la  kuzalisha malisho ya mifugo lililopo Vikuge wilayani Kibaha, pamoja Halmashuri ya Chalinze wilayani Bagamoyo kisha kuhutubia mkutano wa hadhara  kata ya Pangani na kuwaomba wakazi wa kata hiyo kuacha tabia ya kuvamia maeneo yaliotengwa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Maendeleo.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na watumishi mbalimbali wa kampuni ya Ranchi ya Taifa ya Mlandizi wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani.
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akifafanua jambo kwenye mkutano wa hadhara  kata ya Pangani,ambapo amewaomba wakazi wa kata hiyo kuacha tabia ya kuvamia maeneo yaliotengwa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya Maendeleo.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)
   Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega  (alienyosha mkono) akiwa ameambatana na watendaji mbalimbali wakikagua upanuzi mkubwa wa maabara ya  kutengenezea chanjo za kudhibiti magonjwa ya mifugo  iliyopo  mji wa Kibaha mkoa wa Pwani.

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wafugaji ambapo aliwahakikishia kuwa hakuna Mifugo itakayopotea  kutokana na ugonjwa  wowote.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega(katikati) akiwa katika picha ya pamoja. 
Muonekano  wa Kiwanda cha chanjo ya Hester Biosciences  kinachojengwa kata ya Tangini wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani.(Picha zote na Emmanuel Massaka,MMG)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...