Kiongozi wa Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi. Hanifa Selengu (kulia) akifafanua jambo kwa Wataalam kutoka Halmashauri ya Mji wa Njombe na halmashauri ya Wilaya ya Njombe katika ujio wa timu hiyo kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.
Afisa Maendeleo ya jamii wa Mkoa wa Njombe Bw. Cassian Nkunga akichangia hoja katika kikao kazi kilichowakutanisha Wataalam kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe na Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa lengo la kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bw.Abraham Kaaya akichangia hoja katika kikao kazi kilichowakutanisha Wataalam kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe na Timu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa lengo la kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji wa Njombe Bi. Enembora Lema akichangia hoja katika kikao kazi kilichowakutanisha Wataalam kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe na Timu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa lengo la kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bw. Averino Chaula akichangia hoja katika kikao kazi kilichowakutanisha Wataalam kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe na Timu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa lengo la kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.
Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw. Hosea Yusto akichangia hoja katika kikao kazi kilichowakutanisha Wataalam kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe na Timu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa lengo la kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Denis Bashaka akifafanua jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha Wataalam kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe na Timu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa lengo la kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.
Afisa Ustawi waJamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) (wa pili kushoto) Bi. Mwanaisha Moyo akifafanua jambo katika kikao kazi kilichowakutanisha Wataalam kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe na Timu kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa lengo la kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.
Wataalam kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati Timu kutoka kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kwa lengo la kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

……………………….

Na Mwandishi Wetu Njombe

Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) wamekutana na Wataalam kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji wa Njombe kwa lengo la kuunganisha nguvu na Serikali ya Mkoa katika kupata namna bora ya kukomesha na mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani Njombe.

Akizungumza katika kikao hicho Mwenyekiti wa Timu hiyo Bi. Hanifa Selengu amesema kuwa Wizara imeuunda Timu hiyo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Mkoa wa Njombe katika kutafuta namna bora ya kukomeshana mauaji ya watoto yaliyotokea mkoani humo na kuwezesha wataalam wa mkoa kwa kushirikiana na wadau kwenda kwa jamii kutoa elimu juu ya kuachana na mila zisizofaa hasa zinazoangamiza watoto.

Ameongeza kuwa lengo la kukutana na Wataalam hao ni kuandaa jumbe maalum zitakazotumika katika jamii ili kutoa hamasha kwao kuzingatia umuhimu wa malezi kwa watoto na kuachana na mila zisizofaa katika jamii elimu itakayowasaidia kutimiza majukumu yao ya kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Akizungumza katika kikao hicho Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Njombe Bw. Cassian Nkunga amewataka Maafisa hao kutoka Idara za Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu kutoa maoni yao ili yawezeshe kutengeneza jumbe maalum zitakazotumika katika jamii ili kutoa hamasha kwao kuachana na mila zisizofaa katika jamii hasa zinazoangamiza watoto.

Akitoa Taarifa ya utendaji kazi ya Idara ya Ustawi wa Jamii kwa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Afisa Ustawi wa Jamii Bw. Averino Chaula amesema kuwa Idara ya Ustawi wa Jamii ya Wilaya imeshirikiana na wadau wa watoto katika kutoa elimu kwa jamii kila mara na waliongeza nguvu kubwa mara baada ya kutokea kwa mauji ya watoto mkoani Njombe.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bw. Abraham Kaaya ameshauri elimu kutolewa kwa jamii kwa kuwataka wanajamii kuvunja ukimya kwa kutoa taarifa ya vitendo vyote vya ukatili dhidi ya watoto.

Kwa upande wake Mwanasheria kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bw. Denis Bashaka amesisitiza suala la kujikita katika kufichua tatizo linalosababisha kutokea kwa mauaji hayo na kuangalia namna bora ya kuzifikia jamii kutoa elimu na kuzingatia Sheria, Sera na Miongozo katika kuandaa jumbe hizo.

Wizara imekutana na Wataalam wao kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii na Elimu mkoani Njombe kutengeneza jumbe maalaum zitakozotumika katika Jamii, Vyombo vya Habari katika kutoa elimu juu ya kuzingatia malezi bora kwa watoto na kuachana na mila zisizofaa hasa zinazoangamiza watoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...