NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

WATU 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Pwani, baada ya kukamatwa na wakiwa na kete 173, puli 19 ,misokoto 88  ya bangi pamoja na wengine wawili wakiwa na kete tano za madawa ya kulevya aina ya cocaine  .

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema, watuhumiwa hao wamekamatwa katika msako unaoendelea mkoani hapo. 

Alieleza, huko Kwamfipa kata ya Kongowe walikamatwa Ramadhani Salehe na Frank Lusasi wakazi wa Mwendapole wakiwa na kete za madawa ya kulevya aina ya cocaine ambapo walikiri kujihusisha na uuzaji wa madawa hayo. Wankyo alisema kwamba, baada ya mahojiano na upelelezi kukamilika wote watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria. 

Aidha watu watano wanashikiliwa na jeshi hilo, kwa kosa la kupatikana na mitambo miwili ya kutengeneza pombe aina ya gongo na lita 65 za pombe hiyo.   Wankyo alitoa rai kwa jamii hususan kundi la vijana kuacha kujiingiza katika uuzaji wa madawa ya kulevya na bangi na kuacha kuvuta bangi kwani ina madhara kwao kiafya. 

Aliwaasa wafanye kazi nyingine ikiwemo ujasiriamali ili kujiepusha na biashara zisizo na tija kwao na ambazo haziruhusiwi kisheria. Pia aliisa jamii kufichua wale ambao wanawatilia shaka kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu ili sheria ichukue mkondo wake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...