NA MWAMVUA MWINYI, PWANI 

OMARY Abdallah maarufu Mboweto (50) mkazi wa Kagera ,Dar es salaam aliuawa na watu waliojichukulia sheria mkononi ,kijiji cha Malale kata ya Vihingo, Mzenga Kisarawe mkoani Pwani,baada ya marehemu akiwa na washirika wenzake wawili kufanya jaribio la kupora pikipiki huko Maneromango. 

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Wankyo Nyigesa alisema, tukio hilo limetokea  usiku wa kuamkia march 15 mwaka huu .

Alieleza, marehemu kabla ya kuuawa akiwa na wenzake wawili wakitumia gari namba T. 613 DFG aina ya carrina walifika Maneromango na kufanya tukio hilo. 

"Baada ya wananchi kuwashtukia ndipo marehemu alikimbiza gari kwa lengo la kukimbia, 

"Walipofika katika cha Vihingo, gari lao lilipata ajali ya kuingia kwenye korongo ambapo waliacha gari hilo na kukimbia ndipo wananchi waliwakimbiza na kumshambulia marehemu kwa silaha mbalimbali za jadi na mawe na kusababisha kupoteza maisha "alifafanua Wankyo. 

Wankyo alieleza, mtuhumiwa mwingine mmoja Abdul Zuberi maarufu Mvidunda (35)mkazi wa Chamazi alikamatwa maeneo ya Sumbwi wakati akijaribu kutoroka. 

Watuhumiwa baada ya kuhojiwa wamekiri kujihusisha na matukio mawili ya uporaji tarehe 14 January mwaka huu huko Kitonga Kisarawe ambapo walipora pikipiki aina ya sanlg namba MC 324 CDL aina ya haoujue mali ya Haruna Goha. 

Wankyo alisema, tukio jingine walilolifanya ni kupora bajaji eneo la Kibuta mali ya Shukuru Ally february 13 mwaka huu. 

Aidha jeshi la polisi mkoani hapo, limewakamata Ally Said maarufu kwa jina la Sober (37)Ramadhani Hamza -Mijoke (40)na Said Ramadhani -Ubwabwa (37)wakazi wa Mwendapole wakijihusisha na uhalifu wa kushusha mizigo katika magari,yanayotumia barabara kuu ya Dar es salaam kwenda Morogoro kwa jina maarufu Lumbesa /Shushashusha. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...