Na Ripota Wetu, Globu ya jamii 

SIKU chache baada ya kurejea Chama Cha Mapinduzi(CCM) Hamisi Mgeja amesema ameamua kwenda kuondoa 'Stress' katika mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti.

 Mgeja aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga amerejea Chama hicho mwanzoni mwa wiki iliyopita akitokea Chadema ambapo alijiunga na chama hicho wakati wa mchakato wa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2015.

 Akizungumza leo kwa njia ya simu Mgeja ameiambia Michuzi Blog kuwa kwa sasa wameamua kwenda kujipumzisha mbuga za wayama baada ya kurejea CCM na hiyo inatoa nafasi kwake na wenzake kutafakari maisha mapya ndani ya CCM baada ya kurejea tena.

"Baada ya kumaliza kazi ya kumsindikiza Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa  nyumbani Monduli na kupokelewa na maelfu ya Wananchi wa Mkoa wa Arusha na Wana-CCM katika tukio la kurejea kwake rasmi na kupewa kadi mpya.

"Tumeamua kuja mbuga za wanyama kupumzika kidogo, ni wakati sahihi kwetu kuondoa 'Stress' za Chadema wakati tunafakari namna ya kushirikiana na Mwenyekiti wetu wa Chama Rais Dk.John Magufuli katika kuleta maendeleo ya Taifa letu,"amesema Mgeja.

Amesisitiza kuwa baada ya kurejea CCM kwa sasa moyo wake umejaa amani tele na kueleza anajihisi mwenye furaha na ameutua mzigo uliokuwa kichwani hasa kutokana na aina ya maisha aliyokuwa anaishi Chadema.

 "Nimekaa Chadema , kuna mambo nimejifunza nikiwa huko.Ndio maana wakati narejea CCM niliamua kuwapa ushauri iwapo  wanataka kuwa Chama cha siasa lazima wabadilike tofauti na hapo watabaki kama walivyo,"amesema Mgeja.

Akizungumzia mwenendo wa siasa nchini Mgeja amesema anampongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo."Hakika Rais wetu mpendwa anafanya kazi kubwa sana ya kuleta maendeleo, ni jukumu letu kumuunga mkono kwa kila hatua."amesema Mgeja.
 Hamisi Mgeja (Katikati) akifafanua jambo wakati anazungumza na makada wenzake wa CCM ambao wameamua kwenda kujipumzisha mbuga ya  wanyama Ngorongoro baada ya kurejea katika Chama hicho akitokea Chadema
 Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Hamisi Mgeja ambaye aliamua kuhamia Chadema na sasa amerejea tena CCM akiwa katika moja ya jengo lililopo katika mbuga ya wanyama Ngorongoro ambako amekwenda kupumzika.
Hamisi Mgeja wa pili kushoto akiwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa(mwenye nywele nyeupe) pamoja na baadhi ya Wana-CCM wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili mkoani Arusha

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...