Na Moshy Kiyungi, Dar es Salaam
Msanii maarufu wa muziki wa R&B wa nchini Marekani Beyonce, ametikisa ulimwengu baada ya kuanzisha dini yake iitwayo Beyism.

Dini hiyo ni ya kuabudu iliyoanzishwa rasmi mwaka 2014, alishirikiana na marafiki zake mjini Atlanta, Georgia nchini humo, akaanzisha kanisa lake liitwalo The National Church of Bey.

Kwa mujibu wa kiongozi muanzilishi wa dini hiyo, Pauline John Andrews, alianza kwa kufungua tovuti ya kuwaita watu kujiunga nao ambapo alifanikiwa kupata wafuasi 12, ndani ya kipindi kifupi wakajitokeza wafuasi wengine 200 kanisani hapo.

“Ni dini halisi inayoongea, yeye Beyonce kuwa ni mungu anayepumua, anayeonekana kila siku” alitamka Pauline.

Baada ya kuanzishwa mjini Antlanta, Dini hiyo ya Beyism imeendelea kutawanyika hadi katika jiji la San Francisco, California, nchini Marekani ambapo katika Kanisa la Grace wanayo misa maalumu ya Beyonce.

Katika kanisa hilo linaloongozwa na mchungaji Yolanda Norton, ambaye anatumia biblia iitwayo Beyble katika mafundisho pamoja na nyimbo zake.

Tayari makanisa yanayomuabudu Beyonce, yanatumia Biblia hizo maalum ziitwazo Beyble.

Yaelezwa kwamba utaratibu unaandalia wa kuchapishwa kwa biblia hizo nyingi zitakazoanza kupatikana bure duniani kote.

Mbali na Beyble, makanisa yanayomuabadu Beyonce hutumia nyimbo zake kama sehemu ya kwaya na kila wimbo na maana yake.

Umetolewa mfano wa nyimbo za Pretty Hurt, ambao ni wa kiroho, Drunk in Love ni wa Uhusiano na Upendo, Heaven ni wa kifo, Blue ni wa wa Watoto, Grown Women ni wa Nguvu na Uhuru, Superpower ni wa Upendo, Mine ni wa Uhusiano na Upendo, Blown ni wa Uhusiano pamoja na No Angel nao ni wa Upendo na Mapenzi.

Beyonce hivi karibuni ameongeza wigo wa dini yake kwa kununua kanisa mjini New Orleans nchini Marekani, lenye thamani ya dola za Kimarekani zipatazo 850,000 (zaidi ya shilingi za Kitanzania Biion 1.7)

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, kanisa hilo lilijengwa mwanzoni wa miaka ya 1990, ambapo linasemekana kuwa na umri wa zaidi ya miaka 100. Kanisa hilo limekuwa halitumiki kwa muda mrefu baada ya waumini wengi kufariki dunia. Kanisa hilo lina ukubwa wa mita za mraba wa 7,500 linasemekana haliko mbali sana na anapoishi dada wa Beyonce, Solange.

Adha Beyonce tayari amekwisha nunua mjengo wa kuishi karibu na kanisa lake.

Dini hiyo ya Beyble, imechota waumini maelfu ambapo inaonesha baadhi ya wafuasi watu maarufu kama akina Kanye West, Mariah Carey, Rihanna Nicki Minaj na wengine wengi.

Wasifu wa Beyoncé unaeleza kuwa alizaliwa Septemba 04, 1981 ni mwimbaji wa muziki wa R & B, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi, mwigizaji na mwanamitindo kutoka Marekani.

Alizaliwa na kukulia Houston, Texas na alihudhuria shule mbalimbali zinazofunza sanaa. Beyonce pia alianza kushiriki katika mashindano ya kuimba na kucheza ngoma akiwa mtoto.

Akiwa na umri wa miaka tisa, alijiunga kwa mara ya kwanza katika shule ya Parker Elementary huko Hounston, Marekani.

Alikuja kujulikana mwishoni wa miaka ya 1990 kama mwimbaji kiongozi wa kikundi cha wasichana cha R & B, Destiny's Child. Kulingana na Sony, mauzo ya rekodi za Beyonce Knowles, yakiunganishwa na yale ya kikundi cha Destiny's Child, yamezidi milioni 100.

Wakati wa kuvunjika kwa kikundi cha Destiny's Child, Beyonce Knowles alitoa albamu yake ya kwanza, Dangerously in Love mwaka 2003, ambayo ilikuwa mojawapo ya albamu za mwaka zilizokuwa na mafanikio zaidi.

Jambo hilo liliashiria uwezo wake wa kufaulu kama msanii kivyake. Albamu hiyo ilikuwa na mafanikio muhimu ya kibiashara, huku ikitoa nyimbo mashuhuri kama "Crazy in Love", "Baby Boy", zilizopelekea kujishindia tuzo tano za Grammy mwaka 2004.

Kutawanyika kwa kikundi cha Destiny's Child mwaka 2005, kuliendeleza mafanikio yake: Albamu yake ya pili, B'Day, iliyotolewa mwaka 2006, ilikuwa namba moja kwenye chati za Bango, na ilikuwa na nyimbo kama "Déjà Vu", "Irreplaceable", na "Beautiful Liar".

Albamu yake ya tatu, I Am... Sasha Fierce, ilitolewa Novemba 2008, ilikuwa na nyimbo kama "If I Were a Boy", "Single Ladies (Put a Ring on It)", "Halo" na "Sweet Dreams".

Beyonce amefikisha idadi ya nyimbo tano zinazopendwa sana miongoni mwa orodha ya nyimbo 100, hivyo kuwa mmoja kati ya wasanii wawili wa kike walio na idadi kubwa ya nyimbo zilizochukua nafasi ya kwanza katika miaka ya 2000.

Mafanikio ya albamu alizoimba akiwa peke yake yamemfanya Knowles kuwa mmoja wa wasanii wanaosifika sana katika tasnia ya muziki.
Msanii huyo amepanua kazi yake kwa kujihusisha na uigizaji na kuidhinisha bidhaa.Beyonce alianza kazi yake ya uigizaji mwaka 2001, aliposhiriki katika filamu ya kimuziki.

Mwaka wa 2006, alishiriki kama mmoja wa wahusika wakuu katika filamu ya malinganisho ya 1981 ya Broadway musical Dreamgirls, ambayo ilimfanya kuteuliwa mara mbili katika Golden Globe Nominations.

Knowles alizindua shirika la familia yake la mitindo,House of Deréon, mwaka 2004, na limekuwa likihusika na kuidhinisha bidhaa kama Pepsi, Tommy Hilfiger, Armani na L'Oréal.

Katika mwaka wa 2009, jarida la Forbes lilimworodhesha Knowles namba nne katika orodha yake ya watu mashuhuri walio na nguvu na ushawishi mkubwa katika dunia, wa tatu katika orodha ya wanamuziki wa hadhi ya juu, na namba moja katika orodha ya juu ya watu mashuhuri wanaolipwa malipo bora zaidi chini ya miaka 30, akiwa na zaidi ya mapato ya dola milioni 87, kati ya 2008 na 2009.

Wasifu wa Beyonce ambaye ni msanii wa muziki wa R&B, unaonesha kuwa mwaka 1990, akiwa na umri wa miaka tisa, alijiunga kwa mara ya kwanza katika shule ya Parker Elementary huko Hounston, Marekani.

Akiwa shuleni hapo ambapo pia hufundisha muziki, Beyonce alikuwa mmoja wa waimba kwaya wazuri.Miaka minne baadae, Beyonce aliteuliwa kuwa kiongozi wa kwaya katika kanisa walilokuwa wakisali wazazi wake la St. John’s United Methodist.

Katika hali ya kuonesha kuwa muziki umo ndani ya damu yake, katika kipindi hicho Beyonce alikutana na rafiki yake, La Tavia Roberson. Wakaamua kutengeneza kikundi cha kuimba na kucheza dansi kiitwacho Girls Tyme, hapo ndipo kukaibuka wasanii sita akiwemo Kelly Rowland.

Baada ya kupitia matamasha mengi, Girls Tyme waliamua kubadili majina na kujiita Destiny’s Child ambapo walibaikiwa kuwa wasanii watatu ambao ni Beyonce Knowles, Kelly Rowlands na Michelle Williams.

Kama Waswahili wasemavyo kuwa “Ivumayo haidumu” badaye kundi hilo liligawanyika kila mmoja akifanya maisha yake.Ni kipindi kirefu sasa Beyonce amefanikiwa kuiteka dunia katika burudani kupitia nyimbo zake , tangu alipoibuka na albamu yake ya kwanza ya Dangerously in Love mwaka 2003.

Beyonce ambaye hivi sasa ni mama wa watoto watatu aliwazaa na rapa mashuhuri Shawn Carter ‘J Z’.


Makala hii imepatikana toka mitandao mbalimbali.Muandaaji anapatikana kwa namba: 0784331200, 0767331200 na 0713331200. 
BEYONCE AKIFURAHIA JAMBO WALIPOKUWA NA MUMEWE JZ

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...