Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha kwa Waandishi wa habari baadhi ya simu zilizokamatwa kwa wafungwa katika Gereza La Ruanda jijini Mbeya.
Habari na Picha na Wizara
ya Mambo ya
Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amemuelekeza Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike kuwasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi askari magereza wanne wanaotuhumiwa kuingiza simu za mikononi kwa wafungwa na kurahisisha mawasiliano kati ya wafungwa na watu walioko nje
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari jijini Mbeya Naibu Waziri Masauni amesema kumekuwepo na tabia ya kuingiza vitu visivyoruhusiwa magerezani ikiwemo simu, madawa ya kulevya huku baadhi ya askari wachache wasio waaminifu wakitumika katika mchezo huo.
“Nimefanya ziara katika Gereza la Ruanda, nimezungumza na wafungwa na kugundua kuwepo kwa simu ambazo mkuu wa gereza alizikamata. Maagizo ya Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli wakati akimuapisha Kamishna Jenerali wa Magereza ni kukomeshwa kwa tabia ya kuingiza simu magerezani ambalo Rias alisema limekuwa jambo la kawaida,sasa haiwezekani maagizo ya kiongozi wa juu kabisa yapuuzwe...Sasa namuelekeza Kamishna wa Magereza kuwasimamisha kazi askari hao wanne na aunde tume kuchunguza kwa kina zaidi tukio hilo” alisema Masauni
Aliwataja askari hao  na vyeo vyao kuwa ni  Longino Mwemezi (Inspekta),  Alexander Mwijano (Stafu Sajenti) Benjamini Malango (Sajenti)  na Ramadhani  Mhagama huku askari wengine wanne wakiendelea kuchunguzwa kutokana na tuhuma hizo.
Jumla ya simu za mkononi tisa zimekamatwa katika Gereza la Ruanda mkoani Mbeya huku zikishikiliwa kwa uchunguzi zaidi wa kubaini watu waliokuwa wanawasiliana na wafungwa hao na aina ipi ya mawasiliano yaliyokuwa yakifanyika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...