Na Shani Amanzi,
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga amewaasa wananchi wa Chemba kuacha tabia ya kupuuza wito wa Viongozi wa Serikali  na taarifa mbalimbali zinazowahamasisha juu ya maendeleo kwani zoezi la usajili  na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa ni kwa manufaa ya kwao.
Odunga aliyazungumza hayo alipokuwa akizindua zoezi la usajili na utoaji  wa vyeti vya kuzaliwa vya watoto waliochini ya miaka mitano(5) chini ya Rita kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na TIGO lililofanyika  tarehe 19/3/2019 katika viwanja vya Godown.
Odunga  alisema "Ifikie mahali suala la hiari litoke na iwe lazima kwani vyeti vya kuzaliwa kwa watoto ni muhimu sana katika maisha yao ya kila siku,kwani  vyeti  vya kuzaliwa vinatumika kwenye uandikishaji kuanzia darasa la kwanza na  Chuo Kikuu kwenye kuchukua mikopo kwa wanafunzi,tumieni  fursa hiyo kwa kuwa awamu ya kwanza ni bure"
Ningependa zoezi hili Watendaji na Wenyeviti waweze kushirikiana nao bega kwa bega  katika kutoa taarifa hasa kwa wale ambao hawajaandikisha watoto wao na kwa wale wanaogoma hatua kali zichukuliwe,pia nawapongeza wakinamama kwa kuweza kuitika wito wa kuwaandikisha watoto wenu kupata vyeti lakini kumbukeni kasi inahitajika zaidi .
Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus H.Mashimba  amesema katika zoezi hilo lilianza na semina kwa Watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Chemba iliyofanyika tarehe 7/3/2019 mpaka tarehe 9/3/2019 na Wahudumu wa afya na watendaji walipata semina hiyo kuanzia tarehe 11/3/2019 hadi 13/3/2019
Aidha zoezi la usajili na utoaji wa vyeti lilianza rasmi tarehe 15/3/2019 na  kuisha tarehe 28/3/2019 na mpaka leo watoto waliosajiliwa taarifa zao kuingizwa kwenye mfumo wa taarifa kwa njia ya simu .
Vilevile Mratibu wa zoezi hilo kwa wilaya ya Chemba Afisa Ustawi wa Jamii wa Wilaya Bi.Euphrezia Anthony amesema zoezi linaenda vizuri pamoja ya kuwa  changamoto hazikosekani.
Ameeleza kuwa Changamoto  wanazokumbana nazo kwenye zoezi hilo ni pamoja na baadhi ya kata kukosekana kwa mtandao,upungufu wa magari 2pamoja na ugeni wa simu za kisasa kwa watendaji na wahudumu wa afya lakini wanajitahidi kuzikabili kwa kuongeza timu ya usajili kwa njia ya simu na kuongeza gari la pili ili kuhakikisha wanakamilisha zoezi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akikabidhi cheti kwa mmoja wa akina mama aliyeshiriki hafla ya uzinduzi wa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto waliochini ya miaka mitano (5) chini ya Rita kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na TIGO lililofanyika Machi 19,2019 katika viwanja vya Godown wilayani humo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Dkt.Semistatus Mashimba akifafanua jambo kabla ya uzinduzi wa tukio hilo kufanyika . 
Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Simon Odunga akizungumza mbele ya baadhi ya Wananchi alipokuwa akizindua zoezi la usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto waliochini ya miaka mitano (5) chini ya Rita kwa kushirikiana na UNICEF pamoja na TIGO lililofanyika Machi 19,2019 katika viwanja vya Godown wilayani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...