NA FREDY MGUNDA,IRINGA. 
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amewataka wanaume kulipa mshahara kila mwezi wake zao endepo watawakataza wake zao kufanyabiashara la sivyo wawaache wake hao wafanyebiashara kwa uhuru. 
 Akizungumza na wanafunzi wa kike wanaotoka kwenye shule zaidi ya saba za wilaya ya Iringa,Kasesela alisema hivyo kutokana na maswali ya wanafunzi hao waliouliza “kwanini wanaume wamekuwa wakiwakataza wake zao kufanya biashara?” 
 Kasesela alisema kuwa wanawake wamekuwa wafanyabiashara wazuri na wenye bahati ya kupata faida na kuweza kuendesha family pamoja na kuongeza kipato cha familia,kumkata wanamke kufanya biashara kunadumisha uchumi wa familia na nchi kwa ujumla. “Naomba niwaambie wanafunzi kuwa mama zenu ndio wamekuwa msingi mkubwa wa kuijenga familia na kuleta maendeleo ya familia pale panapokuwa na maendeleo baina ya baba na mama hapo ndio familia hizo utaona zinavyokuwa na maendeleo” alisema Kasesela 
 Hata hivyo Kasesela alisema,Wanawake wamekuwa waaminifu,watumiaji wazuri wa mikopo,wanajua kupanga bajeti za familia hivyo ukimwacha mwanamke afanye biashara kwa uhuru lazima familia itapata faida kubwa tofauti na ukimyima mwanamke fursa ya kufanya biashara. “Wanaume ndio tumekuwa tukilazimisha kuchukua pesa za mwanamke na kuzitumia vibaya na kuwasababishia hasara wanawake lakini ukiwaacha wafanye biashara utaona wanavyofanya maendeleo kwa kasi kubwa” alisema Kasesela 
 Kasesela aliwapongeza lyra in Africa kwa kuwajengea uwezo wanafunzi wa kike juu ya kuvunja mila potofu za kimila kwa wanawake ili kuwawezesha wanawake kushika nafasi mbalimbali ya uongozi na kujikomboa kiuchumi. 
 “Lyra in Africa mmekuwa mkiisaidia sana serikali ya wilaya ya Iringa kwa kuwajenga uwezo wanafunzi wa kike kwa kuwa kufanya hivyo kunasaidia kuikomboa jamii kwa ujumla hivyo juhudi zetu zinaonekana na mimi kama mkuu wa wilaya nafurahi uwepo wenu” alisema Kasesela 
 Kasesela alisema,lyra in Africa wamekuwa wakiboresha mazingira ya wanafunzi wa kike kwa kuwajengea mabweni kwenye baadhi ya shule za sekondari zilizopo hapa katika wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivyo ni lazima kuwapongeza kwa kazi kubwa wanayoifanya.
 Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la Lyra in Africa mkoa wa Iringa Roserine Malike aliwataka wanafunzi wa kike kusimamia vilivyo ndoto zao katika maisha iliwayumbishwe na wanaume yoyote yule kwa lengo la kutengeneza maisha yao hapo baadae. “Nyie wanafunzi wa kike mnatakiwa kuwa na msimamo katika maisha yenu kwa kipicho cha maisha ili kujenga maisha yaliyo bora na kuwa mfano kwa wanafunzi wengine wa kike kwa lengo la kuikomboa wanafunzi wengine wa kike hapa nchini” alisema Malike 
 Malike aliwataka wanafunzi hao wakike kucha tabia ya kufanya ngono wakiwa bado wanafunzi na kuwasababisha kuharibu ndoto zao wakiwa na umri mdogo na kuongeza kuwa na vijana wengi mtaani wasio na ajira. 
 “Nafikiri mmeona wasichana wengi walipota mimba wakiwa mashuleni wanavyohangaika mtaani kwa kuwa walipoteza ndoto zao wakiwa bado wadogo hivyo mnatakiwa kuwa makini na kudanganywa na wanaume kwenye umri mlionao kwa kuwa starehi hizi zipo tu kila siku” alisema Malike 
 Nao baadhi ya wanafunzi hao wa kike walimweleza mkuu wa wialaya changamoto ya mfumo wa elimu ulivyojikita wanafunzi kutegemea kuajiliwa pindi wamalizapo chuo au elimu yote hivyo wamemuomba kufikisha kilio hicho serikalini ili waangalie mfumo huo upya.

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akitoa ushauri kwa baadhi ya wanafunzi wa kike juu kujikinga na mimba za utotoni ambazo zimekuwa zikiharibu ndoto za wanafunzi wengi wa kike.
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akibadilisha mawazo na wanafunzi wa kike wanaotoka kwenye shule za sekondari zaidi ya saba kwenye wilaya ya Iringa pamoja na viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Lyra in Africa
Baadhi ya wanafunzi wakipata elimu kutoka wa mmoja ya viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Lyra in Africa
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kike wanaotoka kwenye shule za sekondari zaidi ya saba kwenye wilaya ya Iringa pamoja na viongozi wa shirika lisilo la kiserikali la Lyra in Africa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...