Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mtoto cheti cha kuzaliwa baada ya kusajili watoto katika viwanja vya stand mjini Singida baada ya akizindua kampeni ya kitaifa ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Singida na Dodoma Machi 21,2019.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mzazi wa mtoto aliesajiliwa na kupata cheti cha kuzaliwa katika viwanja vya stand mjini Singida
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mtoto cheti cha kuzaliwa baada ya kusajili watoto katika viwanja vya stand mjini Singida baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Singida na Dodoma Machi 21,2019.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na wananchi mbalibali , wazazi na watoto waliopata vyeti vya kuzaliwa na watendaji wa RITA baada ya kuzindua usajili wa watoto kwa mikoa ya Singida na Dodoma katika viwanja vya stendi mjini Singida
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akionyesha kitabu kinachotumika kusajili watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa baada ya kuzindua kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Singida na Dodomajini Singida leo

……………………

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amezindua kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Dodoma na Singida.

Akizindua kampeni hiyo, Dkt. Mahiga ameitaka RITA kuhakikisha inatunza taarifa za watoto wanazozichukua kupitia mtandao wa simu na kuhakikisha zinapatikana pale zitakapohitajika.

“Kuwasajili watoto hawa kwa kasi hii ni vizuri lakini kazi kubwa ni kuhakikisha taarifa hizo zinawekwa na kutunzwa kule zinakostahili na zinapatikana wakati wote”, alisema Dkt Mahiga.

Amesema Serikali itaendelea kulinda haki za msingi za raia wake na ndio maana umeamua kutekeleza mpango wa Usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano kwa kuwa cheti cha kuzaliwa ni haki ya kila mtoto.

Amesema cheti cha kuzaliwa ni alama na vitambulisho wa uraia wa kila mtu na kwamba Tanzania imeamua raia wake wote wawe na utambulisho wao.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mtendaji Mkuu wa RITA bibi Emmy Hudson amesema tangu kuanza kwa awamu ya kwanza ya kampeni hiyo jumla ya watoto milioni tatu wamesajiliwa na kupewa vyeti katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Simiyu, Geita, Njombe, Iringa, Songwe, Mara, Musoma, Lindi, Mtwara, Dodoma na Singida na inakadiriwa hadi kampeni hiyo itakapokamilika mwisho ni mwa mwezi huu zaidi ya watoto milioni tatu na nusu watakuwa wamesajiliwa.

Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi aliahidi kukusimamia Mkoa wa Singida ili uweze kufanya usajili kwa watoto zaidi ya lengo lililorekebishwa la watoto 280,000 ndani ya wiki mbili ambapo alisema hadi kufikia Machi 20 mkoa wake ulikuwa umesajili zaidi ya watoto 180,000

Kazi ya usajili wa watoto hao inafanywa na wasajili wasaidizi ambao wamepewa Mafunzo maalum ya kuingiza taarifa za watoto kwa kutumia simu ya Mkononi na inafanyika katika vituo vyote vya afya na katika ofisi za kata ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi mjini Singida na kuhudhuriwa na viongozi na watendaji wa serikali kutoka mikoa ya Singida na Dodoma wadau wa maendeleo wa UNICEF, CANADA na kampuni ya TIGO ambayo imetoa simu na mtandao wa simu wake unaothmika kufanya usajili wa watoto katika mikoa hiyo nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...