Makampuni ya Tanzania yanayohitaji kuuza bidhaa katika soko la China yamekaribishwa kutumia mtandao ( E-commerce platform)- mall.ca-b2b.com/index ulioanzishwa mahususi kwa ajili ya kuyakutanisha makampuni yanayonunua na kuuza bidhaa mbalimbali  katika masoko ya China na Afrika

Fursa hiyo imeelelezwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya China-Africa E-Commerce ndugu Zhigang Hou alipokutana na Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki leo jijini Chengdu katika jimbo la Sichuan

Mtandao huo ulioanzishwa mwaka jana una makampuni 5000 yaliyosajiliwa kwa madhumuni ya kutafuta bidhaa mbalimbali zinazopatikana barani Afrika. Inatarajiwa kwamba ifikapo mwaka 2021 mtandao huo utaratibu biashara yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 200.

Balozi Kairuki ameyataka makampuni ya Tanzania yenye bidhaa zenye viwango na ubora  unaotakiwa na soko la kimataifa wajisajili katika mtandao huo ili waweze kukutana na makampuni yanayohitaji kununua bidhaa zao. Aidha, wafanyabiashara wanaotaka kununua bidhaa kutoka China pamoja na nchi nyingine za Afrika nao wanaweza kujisajili katika mtandoa huo ili waweze kukutana  na wauzaji mbalimbali.

Makampuni yenye nia ya kupata taarifa za kujiunga na mtandao huo yanaweza kuwasiliana na mratibu:  zhounana@ca-b2b.com










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...