Wakati ujenzi wa barabara ya Mpemba hadi Isongole Ileje mkoani Songwe ukiendelea shule za Msingi na Sekondari tayari zimeonja matunda ya mradi huo kwa kumwagiwa vifaa vya michezo,madawati pamoja na redio za kisasa kwajili ya matumizi ya wanafunzi.
Kampuni ya Kichina GEO Company iligawa vifaa hivyo ikiwa ni kujibu kwa vitendo ombi la Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Joseph Mkude baada ya kuendelea kupokea kero ya kukosekana kwa vifaa hususani vya michezo kwa shule zake.
Akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela aliishukuru kampuni hiyo na akiwataka wanafunzi kujua mataifa rafiki yenye nia njema kwa nchi yetu kwa manufa ya vizazi vijavyo.
Mkuu wa Wilaya hiyo aliwataka wananchi kutobwaga manyanga katikakufanya shughuli za maendeleo wakitegemea kuendelea kupata misaada kama hiyo,bali mipango waliyojiwekea iendelee kutekelezwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mhe. Ubatizo Songa Songa akizungumza kwa niaba ya wananchi aliwataka wazazi na walezi kufanya vitu vingine vyenye manufaa kwa elimu baada ya pengo la madawati na vifaa hivyo vingine kuzibwa kwa  msaada huo.
Wanafunzi wa shule hiyo kupitia nyimbo na mashairi waliweza kuonesha furaha jinsi watakavyoongeza bidii katika masomo na michezo.
Hotuba ya kampuni hiyo  ilihimiza umuhimu wa kuwekeza katika elimu ili kufikia malengo mbalimbali ya kitaifa ambayo yakisimamiwa vema huleta maendeleo na kulipa taifa heshima mbele ya mataifa mengine.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kakoma Wilayani Ileje mkoa wa Njombe wakifurahia vifaa mbalimbali vilivyokuwa vimewasilishwa hapo shuleni kwao tayari kwa makabidhiano.
Sehemu ya vifaa vya michezo iliyopokelewa na baadaye vitagawiwa kwa shule za Msingi na Sekondari wilayani Ileje
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Mwangela (aliyevaa skafu) akipokea madawati na viti 200 toka kwa mmoja wa wakilishi wa kampuni ya Kichina ya GEO Company 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...