Na Mwandishi Wetu, Globu ya Jamii

Bondia nyota wa ngumi za kulipwa nchini, Hassan Mwakinyo anapanda ulingoni jioni hii kuzichapa na Sergio 'El Tigre' Gonzalez wa Argentina katika pambano la kimataifa lililopangwa kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa mikataifa wa Kenyatta. 

Mwakinyo ambaye anadhaminiwa na kampuni inayoongozwa ya michezo wa kunbahatisha nchini, SportPesa Tanzania jana alishiriki katika zoezi la kupima uzito lililosimamiwa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa ya Kenya (KPBC).

Akizungumza baada ya kupima uzito, Mwakinyo ametamba kushinda pambano hilo kutokana na maandalizi aliyofanya chini ya SportPesa Tanzania.Mwakinyo alisema kuwa chini ya kampuni ya SportPesa Tanzania ambayo ilimpatia kocha, Tony Bellew kutoka Liverpool, Uingereza, pia kwa mara ya kwanza alijiandaa kwa ajili ya pambano hilo akiwa nje ya nchi.

Amesema kuwa hawezi kuwaangusha Watanzania na wakazi wa Afrika Mashariki na kuahidi kumchapa mpinzani wake kwa staili ya ‘knockout’ (KO).

“Sina sababu ya kutoa vizingizio kuwa sijajiandaa vizuri. Wadhamini wangu, Kampuni ya SportPesa wameniandaa vzuri sana, kuwa chini ya kocha mzuri na kambi ya kisasa, ili niweze kufanya mambo makubwa zaidi, lazima nishinde pambano hili,” amesema Mwakinyo.

Amesema kuwa hana cha kumuhofia Gonzalez katika pambano hilo ambapo bondia Fatuma Zarika ‘iron’ atakuwa anapanda ulingoni kutetea taji lake dhidi ya bondia nyota wa Zambia, Catherine Phiri.

Zarika kwa sasa ni bingwa wa Baraza la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) wa uzito wa Super bantam kwa upande wa wanawake.Afisa Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya SportPesa, Kelvin Twissa amesema kuwa wanatarajia kuona pambano mazuri nay a kusisimua nkatika usiku wa Jukwaa la Mabingwa na kuifanya mji wa Nairobi si kuwa mji wa kibiashara, bali wa ngumi za kulipwa duniani.

"Katika pambano letu lililopita, mashabiki wa ngumi walionja nusu ya utamu wa Las Vegas inavyokuwa, hii ni fursa na kuthibitisha kuwa Waafrika wanaweza kufanya kama ilivyo Marekani, huu ni mwendelezo wa shughuli za ngumi za kulipwa,” alisema Twissa.

Mbali ya mapambano hayo mawili, pia bondia wa Tanzania, Iddi Mkwera atazipchana na Nichola Mwangi katika uzito wa Super Light wakati Mtanzania mwingine, Pascal Bruno atatinga ulingoni kuzichapa na Raymond Okwiri wa Kenya katika pambano la uzito wa middle.

Pia kutakuwa na pambano la mabondia wanawake, ambapo Sarah Achieng atapigana na Joyce Awino katika pambano la uzito wa Super Light.
 Bondia kutoka Tanzania, Hassan Mwakinyo akitunishiana misuli na Bondia kutoka nchini Argentina, Sergio 'El Tigre' Gonzalez wakati wakupima uzito, watazichapa kwenye Ukumbi wa mikutano wa mikataifa wa Kenyatta. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...